Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na umati mkubwa wa
wananchi wa kata ya Mao waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa
hadhara akiwa ziarani Mkoani Rukwa kuhamasisha kilimo na shughuli
mbalimbali za maendeleo ikiwepo chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto
walio chini ya miaka mitano, elimu, utawala bora na kampeni ya ondoa
nyasi weka bati ijulikanayo kama “Onyaru” Ondoa nyasi Rukwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na wananchi wa kata ya Legezamwendo
Wilayani Kalambo katika ziara yake ya kuhamasisha kilimo bora na
shughuli mbalimbali za maendeleo. Katika kata zote 13 alizotembelea
wananachi walijitokeza kwa wingi ambapo pia walipewa fursa ya kuuliza
maswali na kuwasilisha kero zao. Maswali na kero zao zilipatiwa ufumbuzi
na nyingine kupewa muda kushughulikiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa
Kata ya Mshani kwenye ziara yake ya kuhamasisha kilimo na shughuli
mbalimbali za kimaendeleo Mkoani humo. Wananchi wengine walilazimika
kupanda juu ya miti ili kuweza kupata ujumbe vizuri.
Ziara
hii ya Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa wa Rukwa ilienda sambamba na zoezi la
chanjo ya minyoo na vitamin A kwa watoto waliochini ya miaka mitano.
Pichani ni Dkt. Edina Yesaya ambaye ni kaimu mganga mkuu wa Halamashauri
ya Wilaya ya Sumbawanga akitoa chanjo kwa mmoja ya watoto waliofika
kupata chanjo hiyo. Watoto zaidi ya 2000 wamepata chanjo hiyo katika
kata na vijiji 13 msafara huo ulipopita.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a akisisitizia jambo kwa
wananchi wa kata ya Kilembe. Aliwataka wananchi kwa kushirikiana na
uongozi wa kata na watendaji kushirikiana kuhakikisha miundombinu katika
shule ya Msingi Kilembe inaboreshwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a akimkaribisha kwa shangwe Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ili aweze kuzungumza na
wananchi wa Kata ya Legezamwendo katika ziara yake ya kuhamasisha kilimo
bora na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Muimbaji
wa kikundi cha kwaya cha Last kutoka Kata ya Legezamwendo akiimba kwa
staili ya aina yake huku akisalimiana na viongozi waliokuwepo meza kuu.
Mambo
yalikuwa hivi katika makao makuu ya Wilaya mpya ya kalambo. Wananchi
walifurika kwa wingi. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliwata viongozi na wananchi
wa Wilaya hii mpya kuzingatia kujenga mji wao kwa kuzingatia mipango
miji iliyo bora pamoja na kusisitizia suala la usafi ambapo Mkuu wa
Wilaya hiyo Ndugu Moshi Chang’a ameteua siku ya jumamosi ya kila wiki
kuwa siku ya usafi kwa Mji mzima wa Matai ambao ndio makao makuu ya
Wilaya ya Kambo.
Wananchi walipewa fursa ya kuuliza maswali na kutoa kero zao.
Kaimu
Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bwana Ngindo akifurahia jambo na Kaimu
Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bwana Frank Mateni na Afisa Kilimo
kwenye dawati la uwekezaji Bwana Misasi Marco kwenye ziara hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na madereva wa
bodaboda katika Mji mdogo wa Laela katika ziara yake Mkoani Rukwa ya
kuhamasisha kilimo bora na shughuli nyingine mbalimbali za kimaendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akigawa “Reflectors” kwa
madereva wa bodaboda katika Mji mdogo wa Laela uliopo katika Halmashauri
ya Wilaya ya Sumbawanga ambapo anafanya ziara katika Mkoa huu
kuhamasisha kilimo bora katika msimu huu wa kilimo pamoja na shughuli
nyingine za kimaendeleo. Mkuu huyo wa Mkoa aliwaasa vijana hao kujenga
umoja wenye nguvu kwani utawasaidia pia kupata mikopo mbalimbali.
Aliugiza uongozi wa halmashauri kuwapimia viwanja madereva hao ambao
wapo 22 viwanja ambavyo watavilipia wao wenyewe.
Zaidi
ya asilimia 70% ya wakulima Mkoani Rukwa hutumia jembe la kukokotwa na
wanyama katika shughuli zao za kilimo. Mkulima katika kijiji cha Matanga
akiandaa shamba lake kwa ajili ya kupanda mazao katika msimu huu mpya
wa kilimo cha mvua wa mwaka 2012.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang’a akiwaimbisha wananchi wa Kata
ya Kilembe Wilayani Kalambo ikiwa ni kuwaweka sawa kwa ajili ya
kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyepo kwenye ziara ya kuhamasisha
kilimo bora na shughuli pamoja na miradi mbalimbali ya maenedeleo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – rukwareview blog)














No comments:
Post a Comment