Tuesday, December 4, 2012

WANAOTUMIA MAHINDI NA KARANGA WAPO HATARINI KUPATA SARATANI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini TFDA Bw, Hiiti Sillo akizungumza katika Warsha ya kujadili sumu iliyopo katika baadhi ya Nafaka ijulikanayo kwa jina la Sumu kuvu. Kwa Upande wake Mkurugenzi wa TFDA amesema kuwa wamebaini kuwa tatizo lipo katika Mahindi na Karanga  zaidi ambapo wanaotumia bidhaa hizo wapo hatarini kupata Saratani.Katika Warsha hiyo wamejadili kuwa Mahindi yanapaswa kuhifadhiwa vizuri na pia kama mahindi au karanga zimeharibika na zinadalili ya kama kuwa na Ukungu (Fungis), basi bidhaa hiyo haitafaa kutumiwa kwa binadamu au wanyama. 
 TFDA imekutana na wadau mbalimbali wanaohusika Moja kwa Moja katika masuala ya chakula nchini ili kujadili matokeo ya usafiri kuhusu sumu kuvu (aflatoxin) katika mahindi na karanga kwa Lengo la kupandwa mikakati ya kuitokomeza.

Akifungua warsha hiyo Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dr. Donan Mmbando alisema kuwa anatambua mchango wa wadau mbalimbali na mikakati inayowekwa katika udhibiti wa tatizo hili la sumu kuvu ambalo lipo zaidi katika mahindi na karanga.


tatizo la Sumu kuvu bado halijaeleweka kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa wataalamu, Sumu kuvu katika nafaka  huweza kusababisha  matatizo ya Kansa ya ini, kushuka kwa kinga ya mwili na kuzaliwa na uzito mdogo.


Katika maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, aliwaeleza wajumbe kuwa, Warsha hii imekuja kufuatia utafiti uliofanyika nchi nzima na kupatikana kwa Hali halisi ya tatizo la sumu kuvu nchini na hivyo basi tukaona umuhimu wa kujadili matokeo ya hayo na wadau mbalimbali.  TFDA kwa kushirikiana na Taasisi ya kimarekani ijulikanayo Kama Abt Associates Pamoja na PACA wameandaa warsha hii ili kukubaliana na wadau mbalimbali katika Sekta ya chakula mikakati ya kutokomeza tatizo la sumu kuvu nchini.

Wadau walio shiriki ni Pamoja na wasindikaji vyakula, taasisi za Serikali, watafiti wa vyakula vya binadamu na mifugo na asasi za kimataifa.

Mgeni Rasmi katika Warsha hiyo ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dr. Donan Mmbando akifungua Warsha hiyo iliyofanyika juzi katika Hoteli ya Myfair jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wadau waliohudhuria katika Warsha hiyo

No comments:

Post a Comment