Saturday, December 8, 2012

MKUU WA WILAYA YA MUHEZA AMUWEKA RUMANDE MTENDAJI WA KATAKWA UONGO

MKUU wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subira Mgalu, amemuweka rumande  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ngomeni wilayani hapa Edmund Zongwe, kwa kosa la kumsomea taarifa ya uongo kuhusu maendeleo ya kata hiyo.
 Ofisa mtendaji huyo alikamatwa juzi mchana na mkuu wa kituo cha polisi Mkanyageni na kupelekwa katika kituo kikuu cha polisi Muheza mjini
Hatua ya kukamatwa Ofisa mtendaji huyo wa kata imekuja baada ya mkuu huyo wa wilaya kutoridhika na taarifa ya maendeleo ya kata kutoka kwa Afisa mtendaji huyo.
Alisema kuwa kutokana na hilo lazima Ofisa mtendaji huyo akawekwe rumande siku moja, akitoka bado atakuwa nakesi.
Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya wakati akizungumza naye alimhisi  mtendaji huyo  kuwa amelewa baada ya kusikia harufu ya pombe ambapo aliagiza akapimwe katika hospitali Teule kama ili kubaini kama kweli amelewa.
Kutokana na agizo hilo Ofisa mtendaji huyo alichukuliwa ndani ya gari la DC huku akiwa na mkuu wa Kituo cha Polisi Mkanyageni na Daktari wa kituo cha Afya Mkanyageni hadi hospitali Teule kwa ajili ya kupimwa.
Baada ya kufika huko alitolewa damu, walirudi kutoa majibu ambapo ilielezwa kwamba hospitali ya Teule haina kipimo kinachoweza hali hiyo ya ulevi au la hivyo damu hiyo kuahidiwa kuwa itapelekwa katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili ama KCMC Moshi.

No comments:

Post a Comment