Thursday, December 13, 2012

KAKA WA RAIS KIKWETE AMUWAKILISHA MDOGO WAKE KWENYE MAZISHI: WAOMBOLEZAJI HAWAJARUH


MAZISHI ya aliyekuwa ofisa Usalama wa Taifa (mstaafu) mkoa wa Mbeya RSO Joseph Nelson Mwasokwa, aliyeuwawa usiku wa kuamkia Desemba 9, mwaka huu Jijini Mbeya, yamefanyika katika Kijiji cha Ibungu wilayani Kyela mkoani Mbeya ambapo Kaka wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Alihuduria mazishi hayo kwa kumuwakilisha Mdogo wake.
Kaka wa rais Kikwete Selemani Kikwete akiingia wilayani Kyela kwenye mazishi ya marahamu mzee mwasokwa
Aliyekuwa mkuu wa mkoa mbeya Mwakipesile akiongea na mzee Mwambulukutu kwenye mazishi ya marehemu Mwasokwa

Waombolezaji 


Katika mazishi hayo, Rais Jakaya Kikwete aliwakilishwa na kaka yake Selemen Kikwete ambaye pia alipata nafasi ya kutoa pole kwa waombolezaji.
Waombolezaji katika mazishi hayo hawakuruhusiwa kuuona mwili wa marehemu kwasababu ambazo hazikuweza kufahamika maramoja bali kilichoruhusiwa kuangaliwa ni picha yake iliyokuwa juu ya Jeneza.
Marehemu Mwasokwa alikutwa na umauti baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana wakamkata na kitu kinachosadikiwa kuwa na ncha kali kisogoni ambapo mwili wake ulikutwa umelazwa kifudifudi nje ya geti la nyumba yake eneo la Block T  jijini Mbeya.
Taarifa za Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, zimesema kuwa wauaji wanaonekana kuwa walitumia panga, ambapo marehemu alikutwa na majereha makubwa sehemu za shingoni, kichwani, mabegani na mkono wa kushoto.
Kwa hisani ya Kalulunga

No comments:

Post a Comment