Saturday, December 8, 2012

FAINALI CECAFA-UGANDA 2:1 KENYA; NGASA BOCCO WAKOSA TUZO APEWA SENTONGO


 
Habari via StraikaMkali blog

MAGOLI mawili ya kujifunga kutoka kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, yamewapa wenyeji Uganda (The Cranes) ubingwa wa 13 michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Chalenji) kufuatia ushindi wa 2-1 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala leo.

Kwa kutwaa kombe hilo, ambalo ni la nne kwa kocha wao Bobby Williamson, Uganda imeondoka na zawadi ya kwanza ya kombe na dola 30,000 wakati Wakenya walioshina nafasi ya pili wamepata dola 20,000 huku Zanzibar Heroes iliyoshika nafasi ya tatu imepata dola 10,000.

Nyota wa Uganda, Brian Umony ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Michuano hiyo na tuzo ya kipa bora imekwenda kwa kipa wa Uganda, Hamza Muwonge, ambaye ameruhusu goli moja tu katika michuano yote, ambapo Uganda wameshinda mechi zao zote.

Utata umekuja katika tuzo ya mfungaji bora baada ya kupewa Robert Ssentongo wa Uganda, mwenye magoli manne na kuachwa Mrisho Ngassa na John Bocco waliofunga magoli matano kila mmoja.

Rais wa CECAFA, Leodegar Tenga alikuwapo jukwaani kuwakabidhi zawadi washindi.

No comments:

Post a Comment