Ujenzi wa Bomba la
Gesi la Mtwara umeanza bila ya kuwa na
mipango ya kuhakikisha kuwa kutakuwepo na Gesi ya Kutosha kuisafirisa Hadi Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa Leo na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF
Prf Ibrahim Lipumba wakati akizungumza
na wandishi wa Habari katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.
Prf, Lipumba amesema kuwa, Bomba hilo litakuwa na uwezo
wa kusafirisha futi za ujazo wa Lita 200
wakati uwezo wa Gesi ya Mnazi Bay iliyopo hivi sasa ni futi za ujazo bilioni 80
ambapo amesema kuwa hakuna mpango unaoeleweka
wa kupata futi 120 ili bomba la Gesi liweze kutumiwa kikamilifu.
Amesema Upatikanaji
wa Mkopo waMasharti nafuu kutoka China
wa Kujenga Bomba la Gesi ndio
umeshawishi Serikali kutekeleza Mradi huu haraka bila maandalizi ya uzalishaji wa Gesi ya Kutosha.
Ameendelea Kusema kuwa Mpaka hivi sasa Gesi kiasi cha futi
za Ujazo Trilioni 33 zimegundulika katika
hasa katika bahari yenye kina Kirefu na Kuna uwezekano Mkubwa wa
Kugundua Mafuta.
“Uchimbaji wa Gesi hii bado hauja anza na inawezekana
ikachukua miaka 7-10 kabla ya Shughuli ya uchimbajiw aGesi kukamilika na kuanza
kuitumia ndani ya nchi na kuiuza nje ya Nchi”, Amesema Lipumba.
Ameongeza kuwa CUF wanaitaka Serikali Kutathmini
upya mantiki na faida za Ujenzi wa Bomba hilo na ielewe kuwa Mradi huo
unaweza ukatekelezwa kwa awamu, ambapo wameshauri awamu ya Kwanza iwe kujenga
bomba la Gesi hadi Somanga Kilwa ili kuongeza uwezo wa kusafirisha Gesi ya
SongoSongo kuja Dar es Salaam
Baadhi ya Waandishi waliokuwemo kwenye Mkutano huo leo |
No comments:
Post a Comment