Saturday, December 1, 2012

BQ CONTRACTORS YAZINDUA MASHINDANO YA TENNIS

Mahindano ya Tennes yanayodhaminiwa na Kampuni ya BQ yameanza jana katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Mashindano hayo yanashirikisha wachezaji mbalimbali wa Tenesi wakiwemo wachezaji wanaocheza kwa kutumia Baiskeli (will chair) kuoka katika baadi ya Shule jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Shule zitakazoshiriki katika Michuano hiyo ni pamoja na Jangwani wasichana, pamoja na  Shule ya Pugu ambapo watakuwepo walemavu kutoka katika shule hiyo watakaoshiriki Mashindano hayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa BQ Contractors Limited ambao ndio wadhamini wa Mashindano hayo Eng John Bura  amesema kuwa wameamua kudhamini michuano hiyo kutokana na kampuni yake kujali na kuthamini michezo.

Mshindi atakayepatikana katika mashindano hayo anatarajiwa kupelekwa nchini Kenya kushiriki mashindano ya Tennes yatakayofanyika janury mwakani.

Waziri Mkuu msataafu Mh, Fredrick Sumaye ndiye anayetarajiwa kuwa Mgeni rasmi ambapo atahusika katika Utoaji wa zawadi za washindi watakaofanikiwa kushinda leo hii. 
Huyu ndiye Eng John Bura Mkurugenzi wa BQ contracors aliyejitolea kudhamini mashindano hayo ambapo alisema kuwa  lengo lake ni kukuza mchezo wa Tennis ufahamike kama michezo mingine.

Wachezaji walikuwa wanajiandaa kwa mashindano ambayo kilele chake ni loa ambapo Mgeni Rasmi  atatarajiwa kuja kutoa zawadi kwa washindi.

No comments:

Post a Comment