Thursday, November 22, 2012

TANZANIA IMESEMA IPO TAYARI KUPELEKA WANAJESHI 800 DRC

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Tanzania iko tayari kupeleka kikosi cha askari wake 800 kwenda kupambana na waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), maarufu kama M23. 
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa haari ambapo amesema kuwa askari hao watajiunga na wengine kutoka nchi za SADC  ili wafike 3200 kwa ajili ya jukumu hilo.
Amesema kuwa Wanajeshi hao watasaidia kwenda kulinda mipaka ya DRC na kuzuia baadhi ya miji inayotekwa na waasi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (M23) ambapo mpaka sasa tayari wameshauteka mji wa Goma.

No comments:

Post a Comment