Sunday, November 11, 2012

NAMNA YA KUJIUNGA FREEMASON NA MAANA YAKE

Rihana akionyesha Alama ya Freemason
Kuna idadi kubwa ya watu waliohitaji kufahamu Freemason ni nini baada ya taarifa kuenea kwamba Freemason ni dini ya kishetani na watu wengi maarufu wamo humo wakiwemo viongozi wa nchi na mastaa wengine kama Jay Z, Rihanna, Beyonce, Kanye West, Celine Dion na hata hapa Tanzania june 2012 magazeti ya udaku yaliwataja wasanii kama Diamond Platnums na Jackline Wolper kwamba wamo humo lakini wasanii wenyewe walikanusha.
Clouds TV/Radio kupitia kwa mtangazaji Gerald Hando ilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Sir Andy Chande ambae aliwahi kuwa kiongozi mkuu wa Freemason Afrika Mashariki kwenye nchi za Tanzania, Uganda, Kenya na Seychelles.
Yafuatayo hapo chini ni maelezo aliyoyatoa.
ALIKOANZIA SIR CHANDE:
Sir Chande: Alifika Tanzania mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyia kazi na alikutana na watu wengi ambao walikua wanahudhuria vikao vya freemasons, akaanza kuuliziaulizia na akajifunza mambo kadhaa kuhusu hao watu.

Kwa wakati huo, hao watu hawakua huru kuzungumzia Freemasons kama anavyofanya chande sasa hivi, haswa kabla ya vita ya pili ya dunia.
Sir Chande anasema wakati huo Freemasons ilikua imegawanywa kwenye makundi tofauti, katika mahospitali, shule, na mashirika mbalimbali na kulikua na kundi maalum la freemasons kwa ajili ya matajiri na wafanyakazi wakubwa wa serikali, ukiangalia vizuri wengi wao walikua wazungu na baadhi ya wahindi.
Kundi la kwanza lilikua linaongozwa na watu wa Scotland, makundi mawili yaliyofata yalikua yanaongozwa na waingereza na kundi la nne lilikua linaongozwa na wahindi ambalo kundi la nne ndilo Chande alilojiunga nalo nalo, ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na freemason, aliapishwa rasmi rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 28, kumbuka kwamba masharti ya kujiunga na freemasons ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.
Baada ya hapo ndipo alipoanza kupenda Freemasons ambapo pia alipanda cheo na kupewa nafasi ya kuongoza kundi au tawi la freemasons katika nchi nne ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda na sychels na akajiunga na miradi tofauti ya freemasons nchini uingereza yakiwemo mahoteli ya kifahari pamoja na kupewa jukumu la kujenga hoteli mpya ya freemasons nchini Ghana kwenye mji wa Khumasi ambayo ni ya kifahari sana.
Hoteli nyingine ya kifahari alisimamia ujenzi wake iko Zambia.
Sir Andy Chande kwa sasa ni mstaafu wa freemasons, 2005 alistaafu kuwa kiongozi wa Freemasons Afrika Mashariki baada ya kuifanyia kazi kwa miaka 19, kwa sasa haudhurii mikutano ya hizi nchi za Afrika Mashariki lakini anahudhuria mikutano ya Uingireza kwa sababu bado anafanya kazi na baadhi ya mashirika Uingereza.



FREEMASONS NI NINI?
Ni taasisi ambayo ilianzishwa miaka 350 iliyopita katika njia ambayo haikua rasmi ikaja kuhalalishwa miaka 300 iliyopita, hatujui vizuri ilianzishwa vipi ila inaaminika walikua wajenzi wanaojenga mashule, makanisa, wakati ule kulikua hakuna miji mikubwa kama sasa wala mahoteli, na wao walikua wakiishi pamoja na familia zao na wakihama wanahama pamoja, wakaanzisha miradi ya kujenga hoteli ndogo ndogo ili kusaidiana kama wajenzi na kujikwamua kiuchumi, wakawa wanafundishana.. yani kama una ujuzi unamsaidia na mwenzako kujua
.

AnasemaFreemasons sio dini na tukikuta wewe ni mkristo tunakushinikiza ukristo wako, kama wewe ni mhindu unabaki kuwa mhindu, lakini freemasons orijino ilianzishwa na wakristo nchini Uingereza na baadae ikahamia Ulaya, Marekani, Australia na India Freemasons ikaja kuwa kubwa sana”
NCHI ZA AFRIKA AMBAZO FREEMASON NI KUBWA:
Kwa nchi za Afrika Freemasons imekuja kuwa kubwa kwenye nchi kama za Nigeria na Ghana pia Sierra Leone, kwanza aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo Daudi Jawala alikua mmoja wetu.

Freemasons ilianza mwaka 1646 alafu ikaja kuwa rasmi mwaka 1717 lakini kabla ya hapo katikati ilikua inafanywa kimya kimya.

KAZI ZINAZOFANYWA NA FREEMASON
Kazi zinazofanywa sasa hivi na Freemasons ni kufundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa mwenyemwezi Mungu, kwa nchi yako, familia, na nchi unayofanyia kazi hata kama ni ugenini, na kutoa misaada.


Alama nyingine hii hapa

WANACHAMA WA FREEMASONS DUNIANI:
Duniani kote sasa hivi kuna wanachama milioni tatu laki tano wa freemasons na wanachangia dola za kimarekani zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya misaada kila mwaka, yani kwa siku ni zaidi ya dola milioni moja kusaidia afya, elimu vilevile wajane wa wanachama wa freemasons wanasaidiwa ambapo pia ukiumwa na ukiwa na shida yeyote kuna msaada wa bure unapatiwa nakumbuka hata dr Charles Matwali alipoumwa sana, tulimpeleka uingereza kwa matibabu.

JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASONS:
Ili kujiunga ni lazima uwe na umri wa miaka 21, ni hiari kujiunga na pia uwe unamwamini Mungu haijalishi ni Mungu gani, watu ambao hawamuamini Mungu hawaruhusiwi kuwa Freemasons, na lazima uwe mtu mkweli
.

Ni lazima familia yako ikubali pia wewe kujiunga na freemasons kwa sababu freemasons hawatokubali kujiunga kwako kukufanye uwe masikini kutokana na kutoa misaada.
Unapotaka kujiunga ni lazima upeleke maombi yako kwa mtu unaemfahamu ambae yuko Freemasons, au kama hujui mtu unaandika barua baada ya hapo utapewa nakala za kusoma na kuelewa na kamati ya kukuruhusu kuingia kwenye freemasons itakupeleleza wewe na familia yako, na pia watakutembelea nyumbani kuongeana mkeo au mumeo au familia.
Inaweza kuchukua mwaka mmoja na nusu au mwaka kuruhusiwa kujiunga na freemasons baada ya kupeleka maombi, ambapo hapo ni kukubaliwa tu, baada ya hapo ili uwe freemason kamili kuna vyeo vitatu ambavyo tunaviita degrees ambavyo ni lazima uvikamilishe jambo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili.


BAADA YA KUJIUNGA:
Pia unatakiwa kujifunza vitu vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya ibada za freemasons kwa sababu tukiwa pamoja tunavyozungumzia sifa za kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.

KUHUSU FREEMASON YA UINGEREZA:
Acha nizungumzie Freemason ya Uingereza ambayo mimi ni mmoja wao, Makao makuu yako London kwenye barabara inaitwa great queen street, Mkuu wa Freemasons Uingereza ni binamu yake malkia Elizabeth ambae tunamuita Grandmaster.
Kazi zote zinazofanyika na Freemasons zinaendeshwa kutoka kule, kwa mfano mv bukoba ilivyozama nilipiga simu kule kuomba msaada wakatuma pound elfu 10 ingawa na sisi hapa tuna kitengo chetu cha misaada ambayo kilichangia, maamuzi ya misaada mikubwa yanatoka Uingereza.
Kuna mahoteli ya freemasons Uingereza, Scotland na Ireland na katika nchi zilizokua za kisovieti zamani, tuna mahoteli duniani nzima ambapo kama upo kwenye freemasons ya Dar es salaam unaweza kuhudhuria vikao kwenye yeyote kati ya hizo hoteli duniani tunazomiliki ambazo zinatumika pia kama kumbi za mikutano yetu ili mradi wawe na uthibitisho kwamba wewe ni mmoja wetu.
Watu wengi huwa wanasema ni taasisi inayofanya mambo yake kwa siri lakini ukweli ni kwamba siri pekee iliyopo ni jinsi nitakavyokutambua kama wewe ni mmoja wetu, vingine vyote viko wazi na vinapatikana hata kwenye internet na unaweza kwenda kwenye maduka ya vitabu kote afrika mashariki hata uingereza ukapata nakala zote za freemasons ikiwemo hata maneno tunayosema tukifanya ibada zetu.
Kwa afrika Mashariki makao makuu ya freemasons yako Nairobi Kenya kwa sababu aliechukua nafasi yangu yuko Nairobi na pia makamu wake yuko Nairobi, Kuna majumba 50 ya freemasons Afrika Mashariki
Ingawa makao makuu yako Nairobi, jumba la Dar es salaam linajitegemea lenyewe na tunafanya miradi yetu na kusajili watu wetu hapahapa, hatuingiliwi na ofisi ya Nairobi, maamuzi yetu yanafanyika hapa hapa.


jengo la Free Masson lililopo Dar es Salaam
Story via Millard Ayo

3 comments:

  1. Welcome to brotherhood Illuminati where you can become
    rich famous and popular and your life story we be change
    totally my name is Dan Jerry I am here to share my
    testimony on how I join the great brotherhood Illuminati
    and my life story was change immediately . I was very poor
    no job and I has no money to even feed and take care of my
    family I was confuse in life I don’t know what to do I try all
    my possible best to get money but no one work out for me
    each day I share tears, I was just looking out my family no
    money to take care of them until one day I decided to join
    the great Illuminati , I come across them in the internet I
    never believe I said let me try I email them.all what they
    said we happen in my life just started it was like a dream to
    me they really change my story totally . They give me the
    sum of $1,200,000 and many thing. through the Illuminati I
    was able to become rich, and have many industry on my
    own and become famous and popular in my country , today
    me and my family is living happily and I am the most
    happiest man here is the opportunity for you to join the
    Illuminati and become rich and famous in life and be like
    other people and you life we be change totally.If you are
    interested in joining the great brotherhood Illuminati.then
    contact him +2348106618681 or for more information +1(705)8062021
    email:illuminatibrotherpowerful@gmail.com or you need my assistance
    email:danjerry04@gmail.com...

    ReplyDelete
  2. Habari zenu, nipo hapa kushuhudia, jinsi nilivyo kuwa mwanamitindo tajiri na maarufu duniani mwenye mafanikio makubwa, nimekuwa nikipitia magumu miaka nenda rudi, tangu nilipofiwa na wazazi wangu wote wawili, sikuweza kuendelea zaidi na mshikaji wangu kutokana na Suluhu la kifedha basi, hadi miezi mitano iliyopita, nilimaanisha rafiki ambaye aliniingiza kwenye familia ya freemason, mwanzoni niliogopa kujiunga, kwa sababu nimesoma habari nyingi za uongo kwenye mtandao kuhusu familia ya freemasonry, na ambayo sasa ninaijua. hiyo sio kweli, zote zilikuwa habari za uongo, na napenda kutumia fursa hii kusema asante sana kwa familia ya freemason, ndugu wote wa familia hii, nawashukuru sana kwa support mnayonipa, na kwa waliodhani familia ya freemasonry ni mbaya, haijui sheria na kanuni za huyu jamaa, tafadhali acha kuhukumu ulikuwa hujui, na acha kusambaza habari za uongo, kama una nia ya kuwa mwanachama ufurahie. faida za familia ya freemasonry, contact off anuani icial hapa chini kwa taarifa zaidi.

    WhatsApp; +31 687 329 133
    Barua pepe; info.masonic.oregon@email.cz
    Barua pepe; info.masonic.oregon@gmail.com
    Au soma zaidi kuhusu sisi kwenye kiungo cha ukurasa wa Facebook; https://web.facebook.com/infomasonicoregon

    ReplyDelete