Wednesday, August 8, 2012

WASANII WAMWAGA MACHOZI BAADA YA KUBAINI WEZI WA KAZI ZAO

Msanii  MOHAMED 'NICE'  akilia baada kukuta kazi zake zikiuzwa katika moja ya duka kwenye mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo jana.

Hili ndilo duka lililokutwa likiuza CD Feki za kazi za wasanii

KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa wasanii wanaotoa kazi hizo
Msemaji wa Kampuni ya Steps  Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashirikiana na wasanii wenyewe kukamata kazi zao maana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubiri kazi za wasanii ili waweze kujitengenezea faida bila jasho, ameiomba serikali kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo
Mmoja wa wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na Dvd ndiyo inakuwa imechakachuliwa huku akiangua kilio na kusema wasanii  wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki chochote. Na www.burudani.blogspot.com