Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa akiongea na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Holidey Inn wakati alipopokea
Hundi ya kiasi cha Shilingi milioni 26 kutoka Tigo kwa ajili ya kuchangia
Madawati katika Shule za Msingi 5 kutoka wilaya mbili Njombe na Makete zilizopo mkoani Iringa
ambapo alisema kuwa shule zitakazo faidika ni Maendeleo watapata madawati 135,
Umoja 196, Kumbila 200, Makonde 152 na Mbela 37. Aliongeza kuwa shule hizo
zimechaguliwa kulingana na kuwepo kwa
haja kubwa zaidi ya Madawati wakwanza
kushoto ni Kaimu Meneja mkuu wa Tigo Bw,
Andrew Hadgson watatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya kupekea michango ya
kusaidia katika sekta ya Elimu Hassan Maajar Trust Zena Tenga wane kwenda kulia ni Mwenyekiti wa
kamati madawati Balozi Betha Somi wamwisho ni Dkt, Sinare Yusuf Sinare
Mwenyekiti wa kamati wa ukusanyaji Fedha taasisi ya Hassan Maajar Trust .
|