Yule
mwanamke wa Sudan ambaye anasubiri kutumikia adhabu ya kifo baada ya
kuisaliti dini yake, amejifungua mtoto akiwa gerezani karibu na mji wa
Khartoum kwa mujibu wa mwanasheria wake.
Mwanamke huyo Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na mwanaume wa
kikristu na amehukumiwa kunyongwa mapema mwezi huu baada ya kukataa
kuuacha ukristu.
Mwanamke huyo ameruhusiwa kumhudumia mtoto wake huyo wa kike kwa miaka miwili kabla ya kutumikia adhabu hiyo.
Meriam alizaliwa na baba wa kiislamu ambapo ameshtakiwa kwa sheria za
kiislamu sharia. Sudan ina idadi kubwa ya watu wa jamii ya kiislamu
inayoongozwa na sheria za kiislamu.
No comments:
Post a Comment