Saturday, May 3, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIANI KUFANYIKA MEI 5


Kaimu Mkurugenzi  wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Humphrey Kihwelu amesema Mkoani Mbeya sherehe hizo zitafanyika katika Hospitali ya Rufaa Mbeya 

Nawa mikono



Maadhisho ya siku ya kunawa mikono duniani kila mwaka yatafanyika Mei 5 mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi  wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Humphrey Kihwelu amesema Mkoani Mbeya sherehe hizo zitafanyika katika Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Adrian Majembe Mwenyekiti wa Mtaa wa Block T Kata ya Iyela.

Kihwelu amesema kuwa nia ya kufanya sherehe hiyo ni kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kunawa mikono kila wakati mara baada ya kutoka Hospitali na kabla na baada ya kula chakula ili kuepukana na magonjwa ya maambukizi.

Kaimu Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii kuhudhuria sherehe hizo ili kupata elimu juu ya umuhimu wa kunawa mikono elimu itakayotolewa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Aidha amesema Adrian Majembe ni mmoja wa wadau ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa Elimu katika shule mbalimbali Mkoani Mbeya mpango ulionesha mafanikio makubwa.

Hospitali ya Rufaa imekuwa mstari wa mbele kushiriki maadhimisho hayo ambapo mwaka jana yalifanyika katika Hospitali ya wazazi ya Meta na Rufaa sherhe iliyopata mafanikio makubwa baada ya wananchi waliohudhuria kunufaika na elimu iliyotolewa.

Kihwelu amesema mwaka huu wameanza maadhimisho hayo kwa kutoa elimu kwa Hospitali mbalimbali za Serikali na Binafsi na kuonesha mafanikio.


Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment