VANESSA MDEE-#Money14
Muite Vanessa Mdee aka VeeMoney ,ni mwanamuziki pia ni mtangazaji…Mwanadada huyu ndiye mmiliki wa logo ya #Money14 ,ni moja kati ya idea yakipekee katika upande mzima wa design ya tshirt zake,imekaa kimtindo wa tshirt na wakati huo huo kama jezi.watu wengi hata baadhi ya wasanii wenzake wameonekana kuvutiwa na vazi la Vanessa.
DIAMOND PLATNUMZ-WASAFI CLASSIC BABY(WCB)
Diamond Platnumz aka raisi wa wasafi, ndio mmiliki wa brand ya Wasafi Classic Baby(WCB),akiwa kama mwanamuziki ambaye ni maarufu sana EastAfrica na nje ya Africa,baada ya kampuni yake ya wasafi ku-make headlines nchini,bila kuchelewa akaingiza mzigo huu wa nguo za wasafi classic baby,zipo kwa kila design ya maneno hayo ya wasafi,ni moja kati ya logo nzuri sana kuivaa,hapo unakuta kofia,Tshirt hadi viatu vya Wasafi utavipata.
OMMY DIMPOZ –PKP
Ommy dimpoz ndio mmiliki wa kampuni yake binafsi inayoitwa PozkwaPoz, ambayo ndio imepelekea brand logo ya PkP,so far ameweza ku-release kofia za PkP na ahadi yake ni kwamba,tusubiri mengi kutoka kwake kwa upande mzima wa mavazi,sababu huo ni mwanzo tu.
WEUSI – NYEUSI CLASSIC
Weusi ni kundi la muziki kutoka jijini Arusha,,ingawa kazi zao nyingi za muziki kwa hivi sasa wamehamishia hapa jijini Dar,kundi linaloundwa na vijana watano, Joh Makini, Lord Eyes, G-Nako, Bonta and Nikki wa pili.Hii ni Logo design yao,ambayo inasimama kama kufanana na jina la kampuni yao iitwayo Weusi,kama rangi halisia ya mwafrika.Nguo zao matata sana ni Tshirts za kike na kiume pia na kofia/snapback,kwa muundo tofauti wa maneno hayo.
IZZO BIZNESS –T UMOGHELE25
Izzo Bizness msanii maarufu wa mtindo wa crank hapa bongo,anayepeperusha vizuri bendera ya huko alipotokea jijini mbeya,Izzo naye anamiliki design logo ya TUMOGHELE 25,huku namba 25 ikiwa ni namba ya muhimu sana kwake,tarehe 25 ndiyo siku alipopigiwa simu na master J kumuita aanze kurekodi,kuanza kazi rasmi, na tarehe ya 25 ni siku yake ya kuzaliwa.Ukiangali ni moja kati ya design kali sana na yakipekee ya tshirt ,tshirt hizi zilitoka na kuambatana na video iliyopewa jina la Tumoghele.
No comments:
Post a Comment