Saturday, April 26, 2014

Utafiti, Huu Mkoa Unaongoza Kwa Maambukizi Ya Ukimwi Tanzania

 

Maambuki ya Virusi vya Ukimwi [VVU] Nchini Tanzania bado ni tishio na mkoa wa Njombe unaendelea kuongoza kwa kuwa na maambukizi ya asilimia kubwa zaidi.
Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 kati ya mikoa kumi yenye maambukizi. Mikoa mingine ni Iringa asilimia 9.1, Mbeya asilimia 9.o, Shinyanga asilimia 7.4, Ruvuma asilimia 7.0, Dar es salaam asilimia 6.9, Rukwa asilimia 6.2, Katavi asilimia 5.9, Pwani asilimia 5.9 na Tabora asilimia 5.1.
Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa Tume Ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi [Tacaids] Dk Raphael Kalinga amesema utafiti wa maambukizi ya VVU Kwa wanaume na wanawake Tanzania bara wenye umri wa kati ya miaka 15 na 45 ni asilimia 5.3 .
Kundi linalo ambukizwa zaidi ni akina mama likifuatiwa na vijana na mikakati zaidi ya makundi hayo inaendelea kuboreshwa ili kupunguza maambukizi kwa makundi hayo.
Dk Raphael Kalinga Amesema asilimia 98 ya Watanzania wanafahamu ugonjwa wa Ukimwi lakini kati yao ni asilimia 60 tu ya wanaoelewa namna ya kujikinga na maambukizi hayo.

No comments:

Post a Comment