Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry, akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry, akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga akiwa katika mkutano huo.
Ofisa Habari wa MSD, Etty Kusiluka akiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa
Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward
Terry (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Utendaji na Mipango ya MSD. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga na Ofisa Idara Habari Maelezo, Frank Mvungi.
Mkurugenzi wa
Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward
Terry (kulia), akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga.
Mkurugenzi wa
Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga, akizungumza na wanahabari kuhusu
utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi. Kulia Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry .
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
|
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imesema asilimia 80 na asilimia 95 ya dawa na vifaa vya tiba huagizwa toka nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar
es Salaam na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja
Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry , alipokuwa akielezea kuhusu utendaji
na mipango ya bohari ya dawa (MSD).
Terry alisema bohari ya dawa ipo
chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii iliyoundwa kwa mujibu wa
sheria namba 13 ya mwaka 1993 na inajiendesha chini ya bodi ya
wadhamini.
Alisema kuwa Bohari ya Dawa MSD ina jumla ya kanda tisa nazo ni Mwanza, Tabora, Mbeya, Iringa, Dodoma, Tanga,
Moshi, Mtwara na Dar es Salaam pia ili kuendelea kusogeza huduma karibu
zaidi na wananchi imefungua kituo kingine wilayani Muleba mkoani Kagera
mwezi machi mwaka huu.
Hata hivyo alisema majukumu ya msingi
ya bohari ya dawa ni kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa vya
tiba na vitenganishi vya maabara kwenye hospitali, vituo vya afya na
zahanati za umma pamoja na taasisi zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii.
"Upatikanaji wa dawa umekuwa
ukiongezeka mwaka hadi mwaka kulingana na bajeti ya serikali na katika
ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii katika mkoa wa
Mtwara ya kuangalia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba mwezi Februari
mwaka huu ulionyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika Hospitali
za Wilaya ya Masasi imefikia asilimia 90,"
Bohari ya Dawa (MSD) hununua dawa na
vifaa tiba kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
pia lazima visajiliwe na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wakati
vitenganishi vya maabara husajiliwa na kuidhinishwa na Private Health Laboratories Board(PHLB).
Kabla ya kuruhusu dawa, vifaa na
vitenganishi vya maabara kuingia nchini hukaguliwa na kupimwa kwa
ushirikiano wa taasisi za serikali kama Tanzania Bureau Agency (TBS), Tanzania Government Chemist Laboratory Agency (GCLA) na The Bureau Industrial Cooperation (BICO).
Terry alisema mwaka 2010 MSD ilifanya
jaribio la kwanza la kufikisha dawa moja kwa moja katika vituo vya afya
na hatua hii ilitokana na agizo la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
ambapo zoezi hilo lilifanyika katika kanda ya Tanga.
"Jaribio la kwanza lilifanikiwa kwa
kiasi kikubwa na kupelekea mnamo mwaka 2011-2012 mikoa mingine tisa
kuingizwa katika utaratibu wa kufikisha dawa na vifaa tiba moja kwa moja
hadi hospitali, vituo vya afya na zahanati".
Alitaja mikoa hiyo kuwa ni Shinyanga,
Lindi, Dodoma, Kigoma, Manyara, Rukwa, Pwani, Ruvuma na Dar es Salaam
na pia kuanzia julai 2013 mpango huu wa utoaji huduma katika vituo
vyote ulienezwa nchi nzima.
Terry alifafanua kuwa MSD ni kitengo
cha Serikali cha mikakati ambacho wakati wote kiko tayari kukabiliana na
majanga yanapotokea nchini na bohari ya dawa kwa kushirikiana na
wahisani inaendelea na mpango wa kupanua maghala ili kuongeza nafasi za
kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
Hata hivyo alitaja changamoto
zinazoikabili bohari ya afya kuwa ni udokozi wa dwa unaofanywa na
wafanyakazi wasio waaminifu, uhaba wa viwanda vya dawa na tiba nchini,
baadhi ya vituo vya afya kutoleta maombi ya dawa na vifaa tiba katika
kanda za MSD kwa wakati, fedha kutoka hazina kuja MSD kutofika kwa muda
muafaka ikiwemo ongezeko kubwa la mahitaji kulinganisha na uwezo wa
serikali.
Hata hivyo Terry aliotoa onyo kwa
wafanyakazi waliopo kwenye vituo vya huduma ya afya kuacha mara moja
tabia ya udokozi wa dawa ili kuboresha upatikanaji mzuri wa dawa kwa
wagonjwa katika vituo hivyo vya afya.
|
No comments:
Post a Comment