Mkazi
wa Kata ya Ngara mjini wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera, Bw, Philimoni
Bunziya akimwelezea mwandishi wa habari hizi jinsi alivyomwagiwa chupa
yenye kinyesi na
mtuhumiwa wakati akitoka Mahakamani katika maeneo hayo.
mtuhumiwa wakati akitoka Mahakamani katika maeneo hayo.
Na Daniel Makaka, Ngara
MKAZI
mmoja wa Kata ya Ngara mjini wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera, Bw.
Philimoni Bunziya alijikuta akishambuliwa na chupa iliyokuwa na kinyesi
karibu na nyumbani kwake alipokuwa akitoka mahakamani.
Tukio
hilo limetokea leo Aprili 28 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika
mji wa Ngara ambapo Bwana huyo aliposhambuliwa kwa kutupiwa chupa ya
maji iliyokuwa imetapakaa kinyesi cha binadamu kwa kupigwa mgongoni
kwake na mtu aliyemfahamu.
Amesema
kuwa baada ya kufanyiwa kitendo hicho alichukua chupa hiyo na kuelekea
kituo cha Polisi cha mjini Ngara kwa lengo la kipata msaada zaidi juu
ya swala hilo na baada ya kufika hapo alitoa maelezo na kupewa
RB.NAMBA.NGR/IR/337/2014. Kw ajili ya mtu huyo aweze kukamatwa na kujibu
tuhuma zinazomkabili.
Bw.
Bunziya amesema kuwa tangu aliporipoti Polisi hadi sasa mtu huyo
aliyemfanyia kitendo hicho ambaye alimtaja kwa jina kuwa ni Bw, Mohamed
Khalfani ambaye ana asili ya kiarabu mkazi wa Ngara mjini hajachukuliwa
hatua yoyote ya kukamatwa au kuhojiwa juu ya tuhuma hizo na amelitupia
lawama Jeshi la Polisi wilaya ya Ngara kwa kushindwa kuchukua hatua.
Alieleza
kuwa ameshangazwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kushindwa kumkamata
bwana huyo huku akiwa anafahamika wazi kwa kumtaja kuwa yeye ndiye
aliyefanya kitendo hicho cha kumtupia chupa hiyo.
Hata
hivyo Bw. Mohamed Khalfani alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya
tuhuma hizo alikanusha na kusema yeye hajafanya kitendo hicho kwa kuwa
hana ugomvi wowote na Bw. Bunziya hivyo anashangazwa na tuhuma hizo
nzito.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw, Costantini Kanyasu amesema kuwa hana
taarifa na tukio hilo na kusema kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Ngara hivyo atafuatia na kuhakikisha
swala hilo hilo linapatiwa ufumbuzi.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Bw. George Mayunga
amesema hana taarifa juu ya swala hiyo na kusema atalishughulikia ili
mtuhumiwa huyo akamatwe ili ajibu tuhuma hizo zinazomkabili.
No comments:
Post a Comment