Wananchi wa eneo hilo waki wakiangalia eneo hilo kwa masikitiko
nisiseme sana nikanukuliwa kwa haya ila kila mtu atafakari matamko ya viongozi wetu wanayoyatoa kwenye majanga na matukio mbalimbali yanayogharim maisha ya watanzania wenzetu.
Watu wawili wamefariki dunia
baada ya kuangukiwa na kifusi katika eneo la Mlima Terati lililopo halmashauri
ya jiji la Arusha wakati wakiwa wanapakia moramu kwenye gari aina ya Isuzu
lori jana saa 3:30 asubuhi.
Mmoja wa marehemu hao ametambulika kwa jina la
Joseph Solomoni huku mwingine bado hajafamika mara moja.
Janga hili lililofungua mwaka 2014 ni janga lililotokea ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu kufariki dunia kwa watu 13 katika machimbo ya Moram yaliyoko Moshono jijini hapa ambapo viongozi mbalimbali wa mkoa na sekta ya madini walitoa amri kufungwa kwa machimbo yote yasiyokuwa na kibali wala kufuata sheria za machimbo.

Tukio hilo lililoshtua wengi limezua minong'ono
kuwa "Je tamko la viongozi hao ilikuwa zuga ya huzuni ya ndugu wa marehem
waliouawa kipindi hicho....au ilikuwa siasa za kujitafutia umaarufu??
Tukio hilo lililokuwa kama
janga la kitaifa si la mkoa pekee kila kiongozi wakiwemo hata viongozi wa dola
waliahidi kulifuatilia matamko mbalimbali yaliyotolewa na viongozi kwa kukagua
machimbo yote huku naibu Waziri wa madini Masele akiahidi pia kulivalia njuga
machimbo hayo yasiue tena, lakini matokeo yake leo tunasikia ndugu zetu tena
wameuawa kwa kuangukiwa na ngema.
hivi jamani utendaji wa
viongozi wetu wa kuwatumikia wananchi na kuwalinda ni nguvu ya soda pindi tu
inapofunguliwa gesi hutoka kwa kasi na kutulia baada ya mda mfupi ndivyo na
utendaji ulivyo kuwa unashughulikiwa kwa maneno pale janga linapotokea lakini
vitenda ni adim??
nisiseme sana nikanukuliwa kwa haya ila kila mtu atafakari matamko ya viongozi wetu wanayoyatoa kwenye majanga na matukio mbalimbali yanayogharim maisha ya watanzania wenzetu.
Nanyi viongozi tafakarini
matamko mnayoyataka kuyatoa kama mtaweza
kutekeleza kabla ya kutamka na baadae kuishia mitini kwani mnatuweka katika
chuki na kisasi watanzania mnaotuwakilisha
Blog
hii inaahidi kulifuatilia tukio hili na kujuza muendelezo wake pamoja
na matamko ya viongozi yatakayotolewa na viongozi mbalimbali juu ya
tukio hilo, ukiachilia mbali lile lililoua watu 13 Moshono.
CHANZO: BERTHA BLOG
CHANZO: BERTHA BLOG
No comments:
Post a Comment