Vijana ni nguvu kazi ya taifa, lakini vijana hao hao wanaweza kuwa
chanzo cha taifa kutoendelea na kubomoka. Ubomoaji wa taifa huwa kwa
namna nyingi ikiwemo uvivu, ufisadi, na kadha wa kadha. Lakini hapa,
tuangalie hili la madawa ya kulevya na bangi.
Ferouz (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi |
Kila kukicha kuna wasanii wa maigizo na filamu ambao tunasikia
wamekamatwa na madawa ya kulevya, "unga" katika jitihada za 'kusaka
maisha', wenyewe wanasema kuna ajali kazini. Wasanii hao ambao wengi ni
vijana, na pale wanapoonekana kwenye runinga huwa hamasa kwa wadogo zao
na jamii kwa ujumla, wakipenda kuwa kama wao.
Na mchana huu, maeneo ya Sinza, kuna taarifa ya mwanamuziki aliyetamba kwenye muziki wa bongo
fleva, Ferouz, sanasana kwa wimbo wake wa Starehe, ambao ulikuwa
ukionyesha madhara ya UKIMWI na virusi vya UKIMWI. Ferouz anadaiwa
kukutwa na bangi, na picha ambazo Gospel Kitaa imezipata eneo la tukio, zinamuonyesha akisindikizwa na maafande kunako mbele ya vyombo husika.
Vijana wa Tanzania tuna
shida gani? Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu tunazo, sasa nini shida
zaidi? Ipo haja ya Operesheni ambazo Askofu Sylvester Gamanywa ameitisha
za Takasika iliyomalizika hivi karibuni, na kisha kupokelewa na Operesheni Milikisha,
kuwahusisha pia wasanii wa aina zote, maana wanaonekana kukumbwa na
janga hili kwa sana, vinginevyo, vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa
watakuwa wakijaa jela za ndani na nje, wakiacha wageni kuja kutawala.
Askari wakiwa wamemzingira. |
No comments:
Post a Comment