Sunday, January 19, 2014
FLORA MVUNGI ABARIKI PENZI LA DIAMOND NA WEMA
Mahusino ya Diamond na Wema yameonekana kurudi kwa kasi hasa baada ya party iliyofanyika December 25 pale Leaders iliyowahusisha watoto mbalimbali kusherehekea Xmass na watoto wenzao ndipo kulipoonesha kuchipua upya kwa mahusiano hayo.
Katika siku hiyo ya Xmass wakati Diamond akitaka kuanza kuimba wimbo wake wa Ukimuona alimkatisha Dj na kuwauliza watoto’mimi mchumba wangu nani?’watoto wakawa wanajibu Wemaaa,Ndipo Diamond akawatangazia watoto kuwa ngoja aje mchumba wake wamuone alipopanda jukwaani alikua ni Wema Sepetu.
Watoto walishangilia kuona hivyo sasa pengine walifurahi kuona walichokua wakikitabiri ni sawa ama walifurahia kuona mahusiano juu ya hao mastar wawili wa Tanzania yanaendelea,siku za hivi karibuni bado watu wengi wamekua wakiendelea kuzungumzia uhusiano huo mmoja wapo aliyeamua kupost mpaka kwenye akaunti yake ya Instagram ni mume wa H.baba bibie Florah Mvungi.
Florah alipost picha inayomuonyesha Diamond akiwa kwenye pozi la kimahaba na Wema huku chini akiandika ‘me na mume wangu tunapendana sana but still tunaipenda sana hii couple iendelee kuwepo.Mungu awajalie mapenzi tele wafike malengo all the best darlings.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment