TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE
Kama mojawapo
ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa
yanayowaandama ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi
karibuni, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma
zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya
uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza;
Tuhuma hizo ni pamoja na;
1. Kwamba
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40
ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo.
2. Mwaka
2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni
20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Tarime, kisha akazitoa kwenye chama
kama mkopo na akalipwa.
3. Mwaka 2010,wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais.
4. Mwaka
huo huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa,
alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni.
Idara ya Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo;
1. Hakuna
ukweli hata mmoja katika tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa
kama moja ya mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii
kwamba viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama
hiki kikuu cha upinzani kinachobeba matumaini ya Watanzania katika
kupigania haki zao na kupinga kila
aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.
aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.
2. Matokeo ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.
3. Idara
ya Habari ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan
wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini
kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie
kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.
4. Kwa
uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama,
wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini,
kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati
wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa
malengo yaliyosemwa.
5. Tungependa
kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza
heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo
wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya
kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi
yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi
wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu,
ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko
ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.
6. Taarifa
kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti
wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji,
zitajibiwa kupitia taasisi husika.
Imetolewa leo Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
No comments:
Post a Comment