Yule
Sheikh Mtoto maarufu kama Sheikh Shariff ambaye aliitingisha Tanzania
kwa ufahamu mkubwa wa Qur’an akiwa na umri wa miaka tisa hatimaye
amesalimu amri na kuokoka, katika kanisa la Pentekoste Motomoto jijini
Dar es Salaam.
Sheikh Shariff ambaye jina lake halisi ni Sheikh Shariff Mohamed Mikidadi tayari amebatizwa na kupewa jina jipya la Michael Sylivester Sewando, ambapo hivi sasa analelewa kiroho katika kanisa hilo lililopo Keko chang’ombe jijini Dar es Salaam.
….Licha
ya Sheikh Shariff sasa Michael Sewando kuzaliwa katika familia ya
kikatoliki ya mzee Sylivester Sewando na mama yake Joyce Mokiwa, alisema
alisilimu baada ya kutibiwa maradhi yake na mganga muumini wa dini ya
Kiislamu wakati akiwa mtoto.
Katika
umri mdogo, jambo hilo lilimfanya ghafla ajikute akianza kuipenda dini
ya kiislamu na ndipo aliamua kujiunga nayo, ingawaje wazazi wake
walimpinga vikali.
Alisema
ilibidi aondoke Nyumbani kwao Kawe Ukwamani na kuhamia kwa ndugu wa
kiislamu na kuanza kuswali katika msikiti wa Al Shariff, International
Dawas’ Islamic Centre Kawe Dar es Salaam. (SIDC) alikoingizwa rasmi
katika dini ya Kiislamu.
Alisema
mara baada ya kujiunga na dini hiyo na kuanza kuswali katika msikiti
huo, alijikuta akipata ufahamu mkubwa wa elimu ya Qu’ran pasipo
kufundishwa. Sheikh Shariff alisema anachojua ni kwamba uwezo wa kuijua
Qur’an aliupata kutoka kwa majini 2900, yaliyomuingia baada ya kujiunga
na Uislamu.
Alisema
majini hayo ndiyo sababu pekee iliyomfanya awe mahiri sana katika elimu
ya dini ya kiislamu. Akizungumza na wahadhiri mbalimbali nje na ndani
ya Tanzania huku akifanya miujiza na kuendesha mihadhara mingi ya
kiislam.
Kwa
mujibu wa Sheikh huyo aliyeokoka, maeneo aliyowahi kutoa mihadhara ni
Kawe,Tandika , Mbagala, Njoro, Kilimanjaro, Mwembe tayari nchini Kenya,
viwanja vya msikiti Mkuu wa Jijini na Kampala nchini Uganda.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, Sheikh Shariff alisema aliwahi kuishi chini
ya bahari ya Hindi katika eneo la Maskati, nchini Oman, akifundishwa
mambo mbalimbali na majini. Alisema akiwa chini ya bahari alikuwa
akifundishwa na jini mkuu aliyemtaja kwa jina Lusifa ambalo ni la
Shetani, ambapo alikuwa akilishwa mchanganyiko wa damu za binadamu na
wanyama na mifupa ya farasi.
Sheikh
Shariff au Michael Sewando alisema Lusifa au mkuu wa majini ambaye
alikuwa na umbo la mfano wa mjusi mkubwa, ndiye aliyemfundisha masuala
ya uganga wa kienyeji kwa kutumia vitabu maarufu vya kijini. Mambo
mengine aliyofanyiwa akiwa chini ya bahari ni pamoja na kuwekwa katika
moto mkali kwa muda wa siku saba na baadaye katika baridi kali na giza
totoro kwa siku hizo hizo.
Nakumbuka
nikiwa chini ya bahari ambako naamini ni kuzimu, Lusifa aliamuru kuwa
kamwe nisilitaje jina la mtu aliyesulubiwa msalabani kwa maana yaYesu,
kwa vile jina hilo ni baya na huharibu kazi za kuzimu. Pamoja na mambo
mengine mengi ya ajabu aliyofanyiwa au kufundishwa na Lusifa, alisema
baadaye alihitimu na kupatiwa mikoba mitatu iliyosheheni madawa ya
mitishamba, viungo vya wanyama, binadamu na majoka. Unajua nilikuwa
nafanya masuala ya kuagua watu kiganga huku pia nikiendesha mihadhara
mbalimbali ya kiislamu’’ alisema akionyesha kitambulisho kinachoonyesha
kuwa ni mganga wa kienyeji.
Alisema
katika shughuli zake aliwahi kuwasilimisha wakristo mbalimbali wakiwepo
mapadri na wachungaji, ambapo ameahidi kuwarudisha kwa Yesu baada ya
kuokoka. Aidha alibainisha kuwa aliwahi kuoa majini mawili na
kusababisha ajali zilizopoteza maisha ya watu ili kupata damu na nyama
za majini aliyokuwa akiyamiliki.
Kuhusu
jinsi alivyokutana na Yesu na kuokoka, alisema hivi karibuni wakati
akielekea katika shughuli zake za uganga eneo la Mbagala Mgeni Nani,
miguu yake ghafla ilinasa ardhini na akasikia sauti ya Yesu ikimwambia
kwamba aachane na uchafu wake, ili atakaswe kwa damu yake Yesu lakini
alitaka kupinga.
Alisema
akiwa katika hali ya kupinga sauti hiyo, alitokea mama mmoja aliyekuwa
muislam lakini akaokoka, ambaye alimshauri aokoke na kumuongoza zaidi
hadi katika kanisa la Pentekoste Motomoto lililoko Keko Chang’ombe
alikomkiri Yesu na kuokoka baada ya kutolewa mapepo. Kanisa la
Pentekoste Motomoto linaongozwa na Mchungaji Ibrahimu John ambaye kwa
sasa ndiye baba wa kiroho wa Sheikh Shariff.
Sheikh
Shariff (Michael Sewando) alisema baada ya kuokoka, amekuwa akipata
mashambulizi kutoka kwa majini na wachawi hivyo anaomba msaada wa maombi
kutoka kwa wacha Mungu wote.
SOURCE: MSEMA KWELI
No comments:
Post a Comment