Lori
la mafuta aina ya Scania lenye namba za usajiri T772 BAZ
limetumbukiakwenye mtaro eneo la Kihonda barabara kuu ya Morogoro Dodoma
baada ya dereva wa Lori hilo kushuka na kuliacha gari hilo bila
kulizima na kuwafukuza wezi waliokuwa juu ya tenk la gari hilo
wakishusha mizigo.
"
Dereva wa Lori hili alipofika pale kwenye tuta alishuhudia pikipiki
ikiwasha taa na kuzima aliamua kuongeza umakini na kubani kwamba mmoja
wa abiri aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo alipanda juu ya Tenk na kushusha
maboksi ya Oil ndipo dereva huyo aliposhuka akajisahau kuvuta
'endbrack'hivyo wakati akiwafukuza wezi hao huku Lori hilo lililokuwa
kwenye mtelemko lilitembea bila dereva na kuingia kwenye mtaro
Dereva
wa Lori hilo Bw ldd Hoza alipohojiwa alisema alikuwa akisafirisha
mafuta ya petroli kutoka Dar es salaama kueleka Dodoma na kwamba
alipofika kwenye daraja la Kihonda alipunguza mwendo kwa lengo la
kulipanda tuta lililokuwa eneo hilo la daraja.
Kwa
kawaida dereva unapopunguza mwendo ni lazima uangalie kwenye kioo nyuma
yako kuna nini hivyo nilipoangalia niliona dereva wa pikipiki akiwasha
taa na kuzima nilipochunguza zaidi nikaona mtu yuko juu ya Tenk
akishusha maboksi ya Oil nikashuka na kumfukuza kwakuwa eneo hili ni la
mtelemko gari hili lilitembea lenyewe na kuingia kwenye mtaro na wezi
hao walifanikiwa kuondoka na boksi moja la oil kwa kutumia pikipiki
yao"alisema Dereva huyo ambaye mpaka muda huu huyo hapo eneo la Tukio
No comments:
Post a Comment