Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KIPA hodari nchini, Juma Kaseja leo amesaini Mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga SC kwa dau la Sh, Milioni 40.
Kaseja
amesainshwa na vigogo wa Usajili wa Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb na
Seif Ahmed ‘Magari’ mbele ya Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh Ilala
mjini Dar es Salaam.
Kaseja
sasa anakwenda kuungana na makipa wawili aliowahi kufanya nao kazi
Simba SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’.
Hii
inakuwa mara ya pili Kaseja kusajiliwa Yanga, baada ya awali kusajiliwa
mwaka 2009 akitokea Simba SC ambako baada ya msimu mmoja wa Mkataba
wake kumalizika akaachwa na kurejea Msimbazi.
Kaseja
aliachwa Simba SC mwishoni mwa msimu kwa madai kiwango chake kimeshuka
na amelazimika kuukosa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara, ingawa
sasa baada ya kumwaga wino Yanga anarudi kazini Januari.
Kikubwa
kilichoisukuma Yanga SC kumsajili kipa huyo ni uzoefu wake katika
michezo ya kimataifa na inataka inufaike naye katika Ligi ya Mabingwa
Afrika mwakani.
Kaseja aliibukia sekondari ya Makongo, Dar es Salaam ambako aliitwa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2001 chini ya kocha Mnigeria, Ernest Mokake aliyekuwa akisaidiwa na mzalendo, Juma Matokeyo, wote sasa marehemu. Mwaka huo huo alisajiliwa na Moro United aliyoichezea hadi mwaka 2003 alipohamia Simba alipopiga kazi hadi 2009 akaenda Yanga na kurejea mwaka mmoja baadaye ambako alifanya kazi hadi mwishoni mwa msimu uliopita alipotupiwa virago.
Juma Kaseja akisaini Yanga huku akishuhudiwa na Seif Magari. Nyuma ni Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh |
Kaseja na Bin Kleb, nyuma Abdulfatah |
Kaseja aliibukia sekondari ya Makongo, Dar es Salaam ambako aliitwa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2001 chini ya kocha Mnigeria, Ernest Mokake aliyekuwa akisaidiwa na mzalendo, Juma Matokeyo, wote sasa marehemu. Mwaka huo huo alisajiliwa na Moro United aliyoichezea hadi mwaka 2003 alipohamia Simba alipopiga kazi hadi 2009 akaenda Yanga na kurejea mwaka mmoja baadaye ambako alifanya kazi hadi mwishoni mwa msimu uliopita alipotupiwa virago.
No comments:
Post a Comment