Mwili wa mtu aliyeuawa kikatili kwa
kukatwa kichwa ukiwa katika gari la polisi baada ya kufikishwa katika
hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga leo asubuhi kwa ajili ya
kuhifadhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio mtu huyo
alifanyiwa unyama huo nyakati za usiku wa kuamkia leo ambapo mwili wa
mtu huyo ulitupwa kando ya daraja la mto katusa ambako pembeni yake kuna makaburi katika mtaa wa Tambazi
katika Manispaa ya Sumbawanga.
Mwenyekiti wa mtaa wa Tambazi, Christopher Kwimba alisema kuwa mtu
huyo aliyeuawa anakadiriwa kuwa na umri katika ya miaka 25 na 27 hivyo
ni vigumu kumtambua kwa haraka kutokana na wauaji kuondoka na kichwa
chake.
|
No comments:
Post a Comment