TAMWA,TGNP NA LRHS WAMTAKA PROFESSA JUMA KAPUYA AJIUZULU KUFUATIA KASHFA YA KUBAKA NA KUMUAMBUKIZA UKIMWI MWANAFUNZI WA MIAKA KUMI NA SITA
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania
(Tamwa), kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Kituo
cha Msaada wa Kisheria (LHRC), kimelaani viongozi wanaotumia madaraka
yao, nafasi zao na nguvu zao kisiasa kuwadhalilisha watoto wa kike.
Mashirika
hayo yanayotetea haki za wanawake na watoto, yamesema yamesikitishwa na
habari zilizozoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu
wasichana wawili wanaotafuta haki yao dhidi ya kiongozi wa kiserikali
anayetuhumiwa kuwadhalilisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka
"Mashirika
hayo yanafahamu kuwa vitisho vilivyotolewa na kiongozi huyo
vimewasababishia wasichana hao kuogopa kuishi nyumbani kwao kwa kuhofia
maisha yao," ilisema sehamu ya taarifa ya pamoja ya mashirika hayo.
Iliongeza: “Tunashangazwa kuona hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika wakati wasichana hao wakitafuta msaada," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Valerie Msoka, katika taarifa hiyo.
Masharika hayo yametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuwalinda wasichana hao dhidi ya mtuhumiwa.
Aidha, ili kujenga imani na utawala bora, mashirika hayo yamemtaka mbunge huyo kujiuzulu mara moja.
Alisema
Tamwa, TGNP na LHRC, yanawataka Watanzania kuungana na kupinga viongozi
wanaotumia madaraka yao vibaya. Watanzania wapige vita vitendo visivyo vya haki kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria
No comments:
Post a Comment