Tuesday, September 17, 2013

TCRA YATOA MAFUNZO KWA WAMILIKI WA BLOGS TANZANIA


Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Innocent Mungi akitoa mada wakati wa semina ya siku mbili inayohusisha wamiliki wa magazeti tando (Blogs) kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akielezea namna Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano hapa nchini unavyokuwa kwa kasi wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers),iliyoanza  leo ambapo warsha hiyo inafanyika katika  Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.


Dr Raynold C Mfungahema mkurugenzi wa watumiaji na watoa huduma  kutoka TCRA akitoa akielezea mada juu ya Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii katika semina inayohusisha wamiliki wa Magazeti Tando (Bloggers) na wasimamizi wa tovuti


 Joe Musheru CEO wa kampuni ya Google katika Ukanda wa Afrika akitoa mada kwenye semina inayoendeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itakayofanyika kwa siku mbili ikuhusisha Wamiliki wa Magazeti tando au Blog na wasimamizi wa tovuti hapa nchini


 Joe Musheru .CEO wa Google kanda ya Afrika (hayupo pichani) akielezea mabadiliko ya teknolojia kwa kulinganisha na mabadiliko ya Binadamu wa kale kama ambavyo inaonekana katika picha kwenye Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ikuhusisha Wamiliki wa Magazeti tando au Bloggers na wasimamizi wa tovuti


 Rais wa Google Afrika Joe Musheru akitoa mada kwa wamiliki wa magazeti tando au bloggers na wasimamizi wa tovuti kwenye semina inayohusisha wamiliki wa blogs na wasimamizi wa tovuti kwenye semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)


Baadhi ya Washiriki waliohudhuria katika semina ya siku mbili innayoendeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika semina inayofanyika leo na kesho.

No comments:

Post a Comment