Thursday, September 19, 2013

JB ASEMA WAZI KUWA TANGAZO LA HAKATWI MTU HALIMAANISHI KUWA HAJAENDA JANDO KAMA WATU WAAVYO SEMA


Jb au bonge la bwana kama wengi wanavyomuita ameeleza kukerwa kwake na jinsi sms zinavyozidi kuzagaa mtaani zikimsema juu ya tangazo alilofanya la hakatwi mtu hapa.

Akizungumza na thesuperstarstz jb amesema marafiki zake wamekuwa wakimuonyesha sms ambazo zinaeleza kuwa jb anajinadi katika matangazo kuwa hataki kukatwa wakimaanisha kwenda jando,Kiukweli sms hizo nimeziona ila sijapendezwa nazo sema kwakua mimi si msemaji wa kampuni niliyofanya  nayo kazi ningechukua hatua maana watu wanapotosha maana halisi ya tangazo nililofanya na kuliweka kama la kihuni alisema jb

Msanii huyo mwenye majina mengi amesema kwake sio tatizo maana yeye ni msanii ila anapata wakati mgumu sana kwakua anaamini wanaofanya hivyo wanaharibu maana halisi ya tangazo hilo la hakatwi mtu hapa,pia msanii huyo amesema kwa upande wake yeye anaingiza mkwanja nakuwaacha wakiandika ujumbe usiokuwa na maana kwa jamiii

Amewaasa watanzania kuacha kukaa na kutunga maneno ambayo hayana maana badala yake watumie muda mwingi kuwaza na kutengeza faranga ama mkwanja ili maisha yao yawe ya kupendeza na waweze kuzilea familia zao alimaliza mtumishi huyo wa mungu ambaye hivi karibuni alichaguli kuwa msanii bora wa kiume tanzania. 

Kwa hisani ya Mtandao

No comments:

Post a Comment