HUU NDIO MWONEKANO WA HEMEDY BAADA YA KUPATA AJALI,ANA BANDAGE USONI LAKINI HERENI BADO HAJATOA...
Muigizaji Hemedy Suleiman ambaye pia ni mwanamuziki wa
Bongofleva amefunguka kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya
ya gari na
gari hilo kudaiwa kuharibika. Hemedy alikuwa akimsindikiza Gerry Wa
Rhymes ambaye pia ni msanii maarufu nyumbani kwake Sinza na
kupata ajali
baada ya kugonga kalivati. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Hemedy
ameandika "Namshukuru mungu naendelea vizuri baada ya kupata ajali mbaya
iliyonikuta..ahsanteni kwa dua zenu, kifua tu ndiyo kimeumia na mkono"
Get well soon Hemedy
No comments:
Post a Comment