Mchungaji wa Kanisa Moja wapo la Kipentecoste akichangia Mada ambapo alisema kuwa ili swala la Migogoro ya Kidini iishe kinachotakiwa ni kuungama kwa niaba ya Tanzania Nzima. |
Jumuiya ya Makanisa
ya Kipentecoste Tanzania, wamejiondoa
katika Jukwaa la wakristo Tanzania na kusema kuwa sababu za wao kujiondoa
katika Jukwaa hilo ni kutokukubaliana Ki Imani.
Akizungumza katika Mkutano wao jana uliofanyika katika
Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Askofu Pius Erasto Ikongo
ambaye ni Askofu wa Makanisa ya Mirracle Church in Tanzania amesema kuwa sababu
kubwa ya wao kutokukubaliana na Jukwaa
hilo TCF, ni kwamba hawana Mitazamo sawa
ya Kiimani.
Amesema kuwa, sio kweli kwamba, Wakristo wote wamekubaliana
kwamba swala la Kugawana Mabucha likubaliwe kwa upande wao hawajashirikishwa na
hivyo wamesema kuwa wao Wapentecoste wanapingana na jambo hilo la kugawana
Mabucha.
Askofu Ikongo amesema kuwa, wanamuomba Rais Kikwete aingilie
kati swala la kuchinja kwa kurejea kauli ya zamani ya Rais wa awamu ya Pili
mzee Alli Hassan Mwinyi ya kuruhusu kila mtu achinje na ale kivyake.
Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti katika kikao hicho,
ambaye ni Askofu Mkuu wa Pentecoste Renewal Assembly Wilson Mwafululila, amesema
kuwa, kitendo cha kukataza Mihadhara ya Kidini wao kama Wapentecoste hawaliungi
mkono kwani Mihadhara ni sehemu ya Mahubiri kwao.
Askofu Mkuu wa Pentecoste Renewal Assembly akizungumza na waandishi wa Habari juu ya wao kujitoa katika Jukwaa la Wakristo Tanzania. |
No comments:
Post a Comment