Mwelimishaji Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akijibu swali kutoka kwa mmoja wa wamiliki wa Mgahawa leo katika Seminar iliyofanyika katika Hoteli ya Bluer Pearl jijini Dar es Salaam. |
Wafanya Bihashara wa Migahawa pamoja na Bar leo wamepatiwa
Seminar juu ya umuhimu wa matumizi ya Kifaa cha kielectroniki cha kulipia Kodi.
Akiwaelimisha katika Seminar Hiyo iliyofanyika leo katika
Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, Mwelimishaji Mkuu Mwandamizi wa TRA
Bw, Hamisi Lupenja amesema kuwa, lengo la kukutana na Wafanya bihashara ao ni
Muendelezo wa wao kutoa Elimu kwa wafanya bihashara juu ya Umuhimu wa kulipa
Kodi kidigitali.
Kwa upande wao wafanyabihashara na wamiliki wa Migahawa
wameonekana kufurahia Kifaa hicho kwani wamesema kuwa kitawasaidi wao kujua
kuwa Kodi zao zinafika mahali husika na hivyo kuwaondoa hofu, juu ya kuliwa kwa
kodi zao.
Hamza Abdallah ni Mfanyabihashara anayemiliki Bar eneo la Tandika
jijini Dar es Salaam, ambaye amesema kuwa, wafanyabihashara wengi wanakwepa
kulipa Kodi kwa kuhofia kuzidisha hela
nyingi au kupunguziwa lakini baada ya kifaa hicho kuanza kutumika kitamsaidia
mfanya bihashara kujua kabisa kuwa kodi yake inafika Mahali husika.
No comments:
Post a Comment