Thursday, May 23, 2013

WALE POLISI WALIOMBAMBIKIA MTU KESI YA KUKUTWA NA FUVU LA MTU WAFUKUZWA KAZI

JESHI la polisi mkoa wa Morogoro limewafukuza kazi askari wake watatu wa kituo cha Dumila wilayani Kilosa kwa tuhuma za kumbambikizia kesi mfanyabishara Samson Mwita mkazi wa Dumila kuwa alikutwa na fuvu la kichwa cha binadamu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Fausitine Shilogile alisema hatua ya kuwafukuza askari hao ilifikiwa baada ya uchuguzi kukamilika na askari hao kuonekana kufanya shughuli ya upekuzi kwa mfanyabiashara huyo bila kuwa na kibali kitoka kwa maafisa wao wa kazi.

Aliwataja askari hao kuwa ni mwenye namba D 4807 D/SSGT Sadick wa kituo kidogo cha Polisi Dakawa, E 4344 SGT Mohamed na E 3821 CPL Nuran wote wa kituo kidogo cha polisi Dumila.

Pia alisema uchunguzi wao umebaini kuwa askari hao wamefanya kitendo hicho kwa kushirikiana na raia Rashidi Ally (47)mkazi wa Mbagala jijini Dar Es Salaam.

---
Latifa Ganzel, Morogoro
via JukwaaHuru.com

No comments:

Post a Comment