Mtuhumiwa Bomu Kanisani, Asomewa mashtaka 21
Mtuhumiwa Bomu Kanisani Arusha, Victor Ambrose Calist (20).Joseph Pantaleo, Arusha Tanzania
Arusha kumekucha, mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na
jeshi la polisi baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka
21 ya mauaji na kujaribu kuua.
Kesi ya mshtakiwa Victor Ambrose Calist (20) ambaye ni dereva wa
bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo jijini Arushai amesomewa
mashtaka yake mbele ya Hakimu mkazi, Devotha Kamuzora.

Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji ya watu watatu
waliofariki dunia katika tukio ambalo lililotokea Mei 5, mwaka huu.
Mawakili wa serikali, Haruna Matagane na Zachariah Elisaria wanadai
Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua. Hata hivyo
makosa mengine bado hajatajwa mpaka hivi sasa.
Pia polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni waliokuwa
wakishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo baada ya
uchunguzi uliofanywa na
jeshi hilo kwa kushirikiana na FBI na polisi wa kimataifa (Interpol), kubaini hawakuhusika kurusha bomu katika kanisa hilo.

No comments:
Post a Comment