Thursday, May 9, 2013

TANESCO KUMALIZA TATIZO LA UHABA WA MITA NA NGUZO SIKU SI NYINGI

Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limetoa Taarifa kuhusu hali ya Nguzo na Mita zilizokuwa zimepungua mpaka kukawa na Uhaba wa Vifaa hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema kuwa Uhaba wa Mita za Umeme pamoja na Nguzo ulisababisha Shirika Kushindwa, kuwaunganishia wateja wake waliolipa Gharama za kuunganishiwa umeme.
Mramba amesema kuwa, tatizo hilo lilisababishwa na kuchelewa kwa Vifaa hivyo ambapo amesema kuwa katika kuhakikisha uhaba huo unakatika mpaka sasa tayari Mita 10,600 zimeshaingia kati ya Mita 75,000 ambazo zimeagizwa katika Kampuni ya EDMI ya Singapore.

Ameendelea kusema kuwa Mita hizo 10,600 zitaanza kusambazwa kuanzia leo Tarehe 10/05/2013 kwenda katika mikoa yote nchini Tanzania.

Mramba amesema kuwa,  kampuni nyingine iliyopewa zabuni ya kuleta Mita ni Simba Limited ambayo italeta mita 56,000 ambapo tayari kiasi cha mita 9,864 zimeshawasili Bandarini na taratibu za kuzitoa Bandarini zinaendelea.

Ameongeza kuwa, katika kupunguza uhaba wa Nguzo, Kampuni ya Sao Hill Industries Limited ya Tanzania ilipewa Zabuni ya Kuleata Nguzo 6,358, na tayari imeshaanza kupeleka nguzo hizo tangu tarehe 06/05/2013 ambapo hadi kufikia tarehe 08/05/2013 tayari ilikwisha peleka Nguzo 2400 na inaendelea kupeleka.

 

No comments:

Post a Comment