Thursday, May 9, 2013

SHEKH PONDE AFUNGWA MWAKA MMOJA NJE



Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam, imemfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda, huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru.

 Hakimu wa Mahakama ya kisutu Victoria Nonga ametoa hukumu dhidi ya watuhumiwa Sheikh Ponda na wenzake 49 kwa kuwaachia huru. Katika hukumu hiyo Sheikh Ponda amekutwa na hatia ya kosa moja ambalo hakimu wa mahakama hiyo amemhukumu kifungo cha nje kwa mwaka mmoja. Kwa upande wao Ndugu wa watuhumiwa hao ambao walikuwa wameshitakiwa katika mahakama hiyo waliokuwa wamefurika Mahakaman hapo, baada ya kutolewa kwa uwamuzi huo wamejawa na furaha kubwa

No comments:

Post a Comment