Kuanzia
tarehe 26 Juni hadi 3 Julai, Rais Obama na Mkewe wanatarajia kutembelea
nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. Katika ziara yake hiyo,
Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano
wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa
Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha
ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za
kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.
Rais
atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na
jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa
kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa.
Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na
kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini
mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii
na duniani kote kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment