Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama
Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
Watuhumiwa wengine wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi
Wakili wa Msigwa kulia akiteta jambo nje ya mahakama
WATUHUMIWA 60 wa vurugu kati ya machinga na polisi mjini Iringa akiwemo Mbunge
wa Jimbo hilo, Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa wanafanyiwa
utaratibu wa dhamana baada ya mahakama kukubali kupewa dhamana.
Awali watuhumiwa walisomewa mashitaka matatu huku mbunge akisomewa
shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu.
Watuhumiwa
wote wamekana mashitaka dhidi yao na kwa sasa utaratibu wa dhamana
unafanyika mbele ya mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa,
Mheshimiwa Godfrey Isaya.
Mashitaka
waliyosomewa watuhumiwa ni pamoja na shitaka la kwanza la mbunge ambalo
ni kushawishi kufanya vurugu, huku wengine wote makosa yao yakiwa ni
kufanya mkutano bila kibali, kuharibu mali kinyume na sheria ni
kufanya vurugu.
Kada wa Chadema Frank Mwaisumbe akiingia na viongozi wengine wa chadema
mahakamani hapo huku wafuasi wao wakizuiwa nje ya mahakama
Wafuasi wa Chadema wakiwa wamezuiliwa nje ya viwanja vya mahakama
kuu kanda ya Iringa wakati mbunge alipofikishwa katika mahakamani
mchana huu
Ulinzi mkali kweli kweli
No comments:
Post a Comment