IKIWA ni
siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari Michezo Vijana na Utamaduni
Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya
Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba na msanii
nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’ Ruge ametoa
ya moyoni.
Tanzania
Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada
ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba
na kuleta suluhu.
“Mimi
kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari
tuitwe na watu watusikilize pande zote mbili hasa mlalamikaji na
ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa
akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo
Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka
kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja
wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo”
anasema Ruge.
Wakati
huohuo Ruge ameongeza kwamba tayari ameshafuata taratibu za kisheria
ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady
Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa msanii huyo akiitwa katika vyombo
vya sheria.
Lakini
ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya
sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari
kubwa katika jamii inayotuzunguka anasema Ruge.
Mwanzoni
mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media
Group kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log
yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa
Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na
Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi
wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli
ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila
kupokelewa.
No comments:
Post a Comment