Sunday, May 19, 2013

KUFUTWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA KUTOATHIRI KIDATO CHA NNE


Mwishoni mwa wiki wakati akifungua Mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo, amesema kufutwa kwa matokeo ya kidato cha nne ya awali hakutaleta athari kwa wanafunzi wa kidato cha tano.

Alisema kwamba tayari Serikali ilishabadilisha muhula wa kuanza kwa masomo hayo kutoka Aprili hadi Julai kila mwaka.

Pia amevisihi vyombo vya habari pamoja na wananchi kuvuta subira kwa vile si muda mrefu matokeo mapya ya kidato cha nne yatatangazwa baada ya kukamilika kwa zoezi la upangaji upya wa madaraja.

Kuhusu Fomu za Bodi ya Mikopo ya Vyuo vya Elimu ya Juu, alisema, kutokana na kuchelewa kutangazwa matokeo ya kidato cha sita, Bodi hiyo nayo italazimika kurekebisha kwa kuongeza muda zaidi wa ujazaji wa fomu.

Akatumia fursa hiyo pia kutangaza kuwa maombi ya wanafunzi wa kujiunga na Vyuo vya Ualimu nchini yatatolewa upya mara baada ya kutangazwa kwa matokeo mapya ya kidato cha nne.

No comments:

Post a Comment