Tuesday, May 14, 2013

JUKWAA LA KATIBA KWENDA MAHAKAMANI KUSIMAMISHA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa JUkwaa la Katiba Tanzania Mhe, Deus Kibamba akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao makuu ya Jukwaa hilo jijini Dar es Salaam juu ya swala zima la Mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.
 Jukwaa la Katiba Tanzania Limeitaka Tume ya Katiba kusikiliza Hoja za Wanasiasa, Watu Binafsi pamoja na Asasi zingine za Kiraia ili kuchangia kupatikana kwa katiba inayoweza kukidhi mahitaji ya Watanzania wote kwa Ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Jukwaa hilo yal;iyopo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba amesema kuwa, kwa Mwenendo wa Mchakato wa katiba wa sasa, Katiba itakayopatikana haitoweza kukidhi mahitaji ya Watanzania wote kwani Watanzania wengi hawajachangia katika upatikanaji wa Katiba hiyo.

Kibamba amesema kuwa wao kama Jukwaa la Katiba watakwenda Mahakamani kuiomba Mahakama isimamishe Mchakato Mzima wa Katiba Mpya ili kurekebisha Kasoro zilizopo katika Katiba inayotarajiwa kupatikana.
"Sisi hatuendi mahakamani kuvuruga Mchakato wa Katiba Mpya bali tunakwenda kurekebisha kasoro zilizopo katika Mchakato wa Katiba Mpya, kwani sisi kama Jukwaa tunashabikia sana mchakato wa Katiba Mpya ili Tanzania ipate Katiba yenye Kuwajali watanzania Wote kwa Ujumla", amesema Kibamba.

Ameongeza kuwa, kwa kupitia Timu ya Mawakili wao kumi wakiongozwa na Mwanasheria Nguli wa maswala ya haki za Binadamu, Dr, Rugemeleza Nshala, wanaandaa hoja ndani ya siku saba, kuanzia leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment