Thursday, April 4, 2013

WATANZANIA WASHAURIWA KULINDA AMANI YAO

Mwenyekiti TCD, Mhe, Mbatia
Kituo cha Demokrasia Tanzania TCD kimewataka watanzania Kudumisha Amani kama kawaida ya Watanzania kuwa na Amani.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa TCD  Mhe, James Mbatia amesema kuwa, Migogoro pamoja na Mitafaruku ya kisiasa na Kidini sio kawaida ya Watanzania na kusema kuwa kawaida ya Watanzania ni Amani toka ilipopata Uhuru.

Mbatia amezungumzia pia swala la Mgogoro kati ya Waislamu na Wakristo juu ya swala zima la Kuchinja kitoweo, na kusema kuwa ugomvi kama huo ni wa aibu, na una aibisha Taifa letu kwa Ujumla ulimwenguni kote.

"Nchi yetu sasahivi inaelekea pabaya sana, Amani inaelekea kutoweka, niwaombe Watanzania Chonde chonde tuilinde Amani yetu kwani ndiyo kitu kikubwa tunachoweza kujivunia," amesema Mbatia.

Ameendelea kusema kuwa,  Swala la Kuchinja ni jambo lenye uwezo wa kuzungumzika kwa hivyo hamna haja ya kuwa na Ugomvi, ambapo amesema kuwa kabla ya Mwezi huu kuisha watafanya Mazungumzo na viongozi wa Dini zote kwa ajili ya kuzungumzia swala hilo.

Ameongeza kuwa,hakuna haja ya kuruhusu watu wachache kuweza kupoteza Amani ya Nchi nzima kwa kuchochea au kuwapotosha Watanzania.

No comments:

Post a Comment