STORI NA RASHID MKWINDA-CHUNYA
MWALIMU
Mkuu wa shule ya msingi Muheza iliyopo kata ya Namkukwe wilayani Chunya
Simiton Kaponda anatafutwa kutokana na madai ya kutafuna jumla ya
shilingi 500,000 ambazo zilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Ufundi kukarabati majengo ya shule hiyo.
Akizungummza
katika mkutano wa hadhara kijijini hapo Bw.Mulugo ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Songwe alisema kuwa alikabidhi jumla ya shilingi milioni 5
kwa shule kadhaa za jimbo la Songwe na shule hiyo aliipa sh.500,000.
Alisema
kuwa hata hivyo tangu atoe fedha hizo hakuna kilichofanyika shuleni
hapo ambapo wananchi walidai kuwa Mwalimu huyo ametafuna fedha hizo.
Baada
ya taarifa za ubadhirifu huo Bw. Mulugo aliagiza kutafutwa kwa Mwalimu
huyo ili atoe maelezo ya kina juu ya namna ambavyo fedha hizo zimetumika
lakini hata hivyo hakutokea ndipo Bw. Mulugo alipoamua kuagiza
kutafutwa kwa mwalimu huyo ili atoe maelezo ya fedha hizo.
Hata
hivyo Mwalimu huyo hakutokea katika mkutano huo na kudaiwa kuwa alikuwa
amejificha ndipo Bw. Mulugo alipoamua kuunda kamati ya watu watano
kufuatilia tuhuma hizo na kutoa jibu baada ya siku mbili.
|
No comments:
Post a Comment