Wednesday, April 17, 2013

MAREKANI WAADHIMISHA 151 YA UKOMBOZI WA WATUMWA

Picture
Mama aliejifunga Minyororo akionyesha jinsi watumwa walivyo henyeka, katika gwaride la Maadhimisho 151 ya Ukombozi wa Watumwa katika wilaya ya District of Columbia barabara ya Pennsylvania Avenue, NW Washington DC Nchini Marekani.
“Wilaya ya Columbia wanasherehekea kila mwaka ifikapo tarehe 16 ya mwenzi wa Aprili, “Emancipation Day”, ambapo huadhimisha Taifa kulipigana vita kwa ajili ya uhuru na haki ya usawa chini ya sheria,” DC Meya Vincent Gray alisema kwenye taarifa yake.

“Katika mazingira ya kisasa, Emancipation ni Siku pia inatoa muda wa kutafakari juu ya mapambano ya Wilaya ya sasa ya bajeti kwa uhuru na uwakilishi kamili katika Congress.”


Ukombozi wa Watumwa ni Siku rasmi ya likizo kwa umma jijini Washington DC.

Ni  sherehe kwa gwaride, kuheshimu maadhimisho ya kusainiwa kwa DC Compensated Emancipation Act, ambayo iliwaacha huru Aprili 16, 1962, zaidi ya watuma 3,100 waliokuwa utumwani hapa District of Columbia. Viongozi wa umma, shule na vikundi vya jamii huja pamoja familia na marafiki kwa ajili ya tukio hili, kama lililovyofanyika jana Jumanne Aprili 16,  2013.


Zifuatazo  ni picha alizozipiga Abou Shatry alipojumuika katika siku-kuu hiyo. 

Tizama picha zaidi kwenye blogu yake ya swahilivilla.blogspot.com

Meya wa Wilaya ya District of Columbia Vincent C. Gray akitembea katika gwaride la Maadhimisho 151 ya Ukombozi wa Watumwa katika wilaya ya District of Columbia barabara ya Pennsylvania Avenue, NW Washington DC Nchini Marekani.

Askari waliovalia magwanda ya Civil War wakipita katika gwaride katika wilaya ya District of Columbia barabara ya Pennsylvania Avenue, NW Washington DC 

   
Kina Mama waliovalia mavazi Quality ya kihistoria ya Civil War katika enzi za kitumwa wakitembea kwa madaha katika gwaride la Maadhimisho ya Ukombozi wa Watumwa, Wilaya ya District of Columbia barabara ya Pennsylvania Avenue, NW 
Free DC! Statehood:  kama sign zinavyoonyesha katika gwaride la maazimisho ya Maadhimisho 151 ya Ukombozi wa Watumwa yaliofanyika Siku ya Jumanne April 16 Jijini Washington DC

Baadhi ya wananchi wa DC walivyotokelezeaa na ujumbe wa Yes We Can kuunga mkono The Emancipation Day Parade

Cheif wa swahilivilla akiwa na Tabu Henry Tayor African American aliejivisha minyororo kama mtumwa alieeachiwa huru kwa mazungumzo zaidi tutawaletea alichokielezea wakati alipolonga na  kwa swahilivilla.

Mama Nea Kuumba (wapili kushoto) akiwa na wezake kando ya barabara ya  Pennsylvania Avenue, NW wakiunga mkono Emancipation Day Parade - Washington DC

Mjomba Samuel ambae ni mTanzania anaeshi Washington DC akiwa na famili yake katika gwaride la Maadhimisho 151 ya Ukombozi wa Watumwa katika wilaya ya District of Columbia barabara ya Pennsylvania Avenue, NW Washington DC Nchini Marekani.

Chief wa swahilivilla Abou Shatry akiwa na Mayor wa wilaya ya District of Columbia Vincent C. Gray , kushoto Mrs Helen L. Higginbotham katika parade ya mazimisho ya The District of Columbia Emancipation Day

No comments:

Post a Comment