Thursday, April 18, 2013

KUTOKA KWA ZITTO KABWE,MISHAHARA IMEPANDA KWA ASILIMIA 30


Mishahara ya Watumishi wa Umma imeongezewa Bajeti yake kwa jumla ya tshs 1 trilioni. Hivi sasa Bajeti ya Mishahara (wages and salaries) ni wastani wa tshs 320 bilioni kwa mwezi, nyongeza hii inapelekea Bajeti hii kufikia tshs 403 Bilioni kwa Mwezi. Hivyo tunaweza kusema mishahara itaongezeka kwa asilimia 30. Je watumishi wa kada za chini nyongeza yao itakuwa sawa na watumishi wa kada za juu?
 
Je watumishi kama walimu wafundishao shule za Vijijini kama Mwamgongo - Kigoma, Urughu - Singida au Namasakata - Tunduru mishahara yao itakuwa sawa na Walimu wa Jijini Mwanza, Tanga, Dar na Mbeya kwa mfano? Walimu na Wauguzi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu kwanini hawapewi vipaumbele ili kuweka usawa kwenye mgawanyo wa watumishi kwenda maeneo ya pembezoni kama Kigoma, Mtwara, Lindi, Singida nk? (kuna tofauti ya kuwa pembeni na kuwa pembezoni). Jumla ya Bajeti yote ya Mishahara kwa mwaka 2013/2014 itakuwa tshs 5.04 trilioni kutoka tshs 4 trilioni za mwaka 2012/13......

No comments:

Post a Comment