Tuesday, April 2, 2013

JESHI LA POLISI KINONDONI LILIVYO IMARISHA ULINZI WAKATI WA PASAKA

Hivi ni Baadhi ya Vifaa vya Uhalifu vilivyokamatwa na Police Mkoa wa Kinondoni wakati wa Sherehe ya wiki ya Sikuukuu ya Pasaka jijini Dar es Salaam, ambapo kamanda wa Police Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyele amesema kuwa vijana wake wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 25 wanaotuhumiwa na kujihusisha na ujambazi wa kutumia silaha kwa kutumia Pikipiki na Magari. Kenyela amesema kuwa walifanikiwa kuwakamata  majambazi wanaojihusisha na wizi wa Magari amabpo walikamata Gari lililoibiwa maeneo ya Mtambani aina ya Toyota Rav4 lenye namba T.331 BPK ambapo katika Msako wa Polisi walifanikiwa kulikamata Maeneo ya Tegeta.Kamanda kenyela ametoa Ushauri kwa wananchi watakaoibiwa Magari kutoa Taarifa Polisi Mapema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela akionyesha Ndoano inayotumika kuiba vifaa mbalimbali kama simu na Pesa baada ya Wezi kukata nyavu za Madirisha wakati Muibiwa akiwa amelala ambapo kifaa hicho kilikamatwa kwa wahalifu wakati wa wiki ya Sikukuu, kifaa hicho kimebatizwa jina la Jordan.

No comments:

Post a Comment