.Diwani wa Kata ya Mtibwa Luka Mwakambaya akizungumza na wananchi wa kijiji cha cha kidudwe
Bryceson Mathias, Kidudwe Mvomero.
Diwani wa
Kata ya Mtibwa kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Luka Mwakambaya, katika mkutano wa hadhara uliofanywa Kidudwe
wilayani Mvomero, amewazuia wananchi wake wasichange michango kwa sababu
ya Njaa.
Akizungumza
na wananchi waliofurika mkutanoni hapo Mwakambaya alisema, kutokana na
njaa iliyoikumba Kata hiyo, wananchi wake wasichangishwe michango ya
maendeleo ili fedha chache walizonazo, watumie kununulia chakula wapate
wajikimu hadi mwezi Agosti.
Hatua
ya Mwakambaya ya kutoa Katizo hilo ilitokana na Ugumu wa maisha uliopo
ambapo Debe la Mahindi katika Kata hiyo kwa sasa limefikia Sh. 16,000/-,
hali ambayo imewasababisshia wananchi hao kuwa na wakati Mgumu.
Hata
hivyo Mwakambaya alisema, kila Mtaa, Kitongoji na Vijiji vya Kata yake,
viorodheshe Idadi ya Wananchi wenye uwezo wa kuchangia Maendeleo ili
mwezi huo ukifika waweze kuchangisha Machangizo yenye tija mara moja.
Mwakambaya
aliwanyoshea kidole na kuwaonya watendaji wasiwe Miungu Watu kwa kwa
kuwatoza wananchi, Sh. 10,000/- hadi 15,000/- kama ada ya kuwakamatia
waharifu kabla ya kuwafikisha Polisi.
Katika
Mkutano huo aliyekuwa Balozi wa Kitongoji cha kwa Sungura, Christopher
Laurent Mkonomali (CCM), alitangaza kujiunga na Chadema ambapo alijinadi
akisema “ Mimi na Ubalozi wa CCM sasa basi nimehamia Chadema”. Alisema
Mkonomali.
Aidha
Mkonomali alirudisha Kadi ya CCM Na. AA575657 ya Januari 8, 2008 na
kukabidhiwa ya Chadema Na. CDM.250713 na Diwani wa Viti Maalum Juliana
Petrol ya Machi Machi 26, 2013.
No comments:
Post a Comment