Friday, February 8, 2013

TAAS YAWATUNUKU WATAFITI 110 WA SAYANSI


Rais wa Tanzania Academy of Science (TAAS) Prof,Esther Mwaikambo,  akizungumza katika Hafla ya kuwatunuku watafiti wa Sayansi jana  katika ukumbi wa COSTECH uliopo jijini Dar es Salaam.



CHAMA cha wanasayansi Tanzania (TAAS) Kimewatunuku kwa kuwapa vyeti  watafiti  110   wa sayansi kutoka katika sekta mbalimbali nchini Tanzania.



Akizungumza katika tukio hilo Rais wa Chama hicho Prof,Esther Mwaikambo amesema kuwa , tukio hilo ni la kuwatia moyo kutokana na watafiti kuongezeka tofauti na ilivyokuwa mwanazo ambapo walikuwa watafiti 25 tu.

Prof, Mwaikambo amesema kuwa, lengo lao la kutoa Tunuku hiyo ni ili Taaluma ya Sayansi iweze kujulikana zaidi kuanzia shule za Msingi mpaka kwenye vyuo vikuu ambapo watafiti hao watakuwa wakitoa Semina mbalimbali kwenye Shule juu ya Umuhimu wa Sayansi.

Alielezea changamoto inayowakumba kuwa ni, kutokuwepo kwa kamusi ya Sayansi itakayowawezesha wanasayansi kujua maneno  Magumu yaliyopo katika somo la  Sayansi hasa katika shule za Msingi na Sekondari hata vyuo ambapo wanafunzi wanakumbana na Matatizo hayo.

Kutokana na Changamoto hiyo Prof, Mwaikambo amesema kuwa,  Chama kina mpango wa Kutengeneza kamusi itakayokuwa  inatafsiri maneno magumu ya Kisayansi, ili wanafunzi waweze kuelewa sayansi kwa undani zaidi.

“Kweli tunachangamoto ya Ukosefu wa Dictionary lakini chama kipo njiani kutengeneza lkamusi ya Kisayansi ambayo tunatarajia ikamilike hivi karibuni kwani tayari tumesha andika Mradi wa kuomba msaada wa Kamusi hiyo”, amesema Mwaikambo.

Katibu wa  Royol Society iliyopo London  Prof Martin Poliakoff akielezea machache juu ya Utafiti wa kisayansi nchini London katika Warsha hiyo.

Mgeni Rasmi, ambaye ndiye Muasisi wa TAAS na pia ni mjumbe wa  TAAS prof, Mathhew Luhanga akimkabidhi cheti mmoja wa Watafiti wa Sayansi.


Baadhi ya wahitimu kwenye picha ya pamoja wakiwa na vyeti vyao baada ya kutunukiwa.

wahitimu wakishangilia kupokea vyeti vyao

No comments:

Post a Comment