Monday, February 4, 2013

STAR TIMES KUWALEGEZEA WATEJA WAKE NAMNA YA KUPATA VIN'GAMUZI ,, SASA MTEJA ANAWEZA KUJIPATIA KING'AMUZI KWA MKOPO

Afisa Masoko wa kampuni ya Star Times Bw, David Kisaka akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao Makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amezungumzia juu ya huduma mpya ya Kampuni hiyo kwa wateja wake itakayomwezesha Mteja wa Star Times Kukodisha Decoda hizo.
'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
 Kampuni ya Star Times imetambulisha huduma ya kukodisha Decoder kwa wateja wake ili kujipatia huduma za Kidigitali.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, David Kisaka amesema kuwa,ili Mteja aweze kukodisha kin'gamuzi hicho atatakiwa kulipa Shilingi 39 elfu ikiwa kama dhamana ya Decoder na shilingi 6000 kama ada ya kukodisha Decoder ambapo Mteja atajipatia Decoder, Kadi ya Decoder, Nyaya Zake antena ya ndani kijitabu cha maelekezo na Boksi na mteja ataweza kuona channeli 15 zikiwemo za kienyeji.

Ameendelea kusema kuwa Promosheni hiyo, itaanza kutumika siku mteja atakayo kudisha Decoder na itadumu kwa mwaka mmoja 1-5 ambapo mteja ataweza kuongeza muda wa ukodishwaji wa Decoder hata baada ya miaka mitanokupita.
Bw, David Kisaka akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari.

No comments:

Post a Comment