Wazee wa Mtwara
Mikindani leo wameongea na waandishi wa habari kataika ukumbi wa habari Maelezo
kuelezea matakwa yao kwa Serikali juu ya Swala zima la Gesi ambayo inapatikana
katika Mkoa wao.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake Mzee Selemani Mademu amesema kuwa wanaitaka
Serikali kuhakikisha kuwa Gesi inawafaidisha wao kwanza kabla ya kwenda
kuwafaidisha wengine.
Amesema kuwa wao
wametumia Gharama zao wenyewe ikiwa ni pamoja na kuuza Mbuzi wao ili wapate
nauli ya kuja kuitetea Gesi yao kwa manufaa ya wanamtwara wote kwa Ujumla.
Ameendelea kusema kuwa, wanaitaka serikali ihakikishe kuwa
kituo cha kusafishia Gesi kinajengwa mkoani Mtwara kwani kuna bandari yenye
kina kirefu kwa ajili ya Kazi hiyo na amesema kuwa wanaitaka serikali katika kutekeleza swala hilo ifanye vitendo kwanza na sio ahadi
kama ilivyozoeleka.
“Tumechoshwa na ahadi za Serikali na kwa hili hatuhitaji
tena ahadi tunataka vitendo la sivyo Gesi haitoki Mtwara tutazidi kuandamana,
tuna rekodi ya ahadi tuloyo ahidiwa na Serikali na hazijatekelezwa mpaka leo
kama vile: Barabara, Umeme, kuimarishwa kwa Bandari, Mikopo
kwa ajaili ya Ujasiriamali, viwanda vidogo kwa ajili ya Kubangua korosho
n.k kwa hivyo sisi tunataka vitendo tu,
tushachoshwa na ahadi”, amesema Mademu.
Serikali pia imetakiwa, kutimiza ahadi ya kujenga viwanda
kama vya Mbolea na Saruji kama ilivyo ahidi kwa wanaMtwara jambo ambalo
litawapa Matumaini yasiyokuwa na Shaka
kuhusu kupata Ajira, pamoja na kuratibu mchakato mzima wa Matumizi ya Gesi kwa
kuwashirikisha mikoa ya kusini kwa hatua Zote na kwa uwazi.
Aidha wameitaka Serikali kujenga kituo cha kufua Umeme Power
Plant Mtwara.
Wazee hao pia wamekanusha taarifa za Mwenyekiti wa
NCCR-MAGEUZI Mhe, James Mbatia za kuwa
alishushwa Jukwaani tarehe 13/01/2013 na kusema kuwa jambo hilo halina ukweli
wowote.
Hawa ndio wazee kumi kutoka Mtwara wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Habari maelezo jijini Dar es Salaam |
Mzee Selemani Mademu akisoma Tamko kwa niaba ya wenzake |
No comments:
Post a Comment