1. MWAKA 2006 nikiwa tanga nilitoroka
shule asubuhi nikamfukuzia Mtangazaji wa Clouds Fm ya jiji Dar es
Salaam, Hamis Mandi 'B-12' aliyekuja Tanga nadhani kwenye show ya Park
Lane!! am not sure, nikamkuta ameshapanda basi na anataka kuondoka
ikanibidi nikadandia basi na mimi na kuanza kumtafuta miongoni mwa
abiria, kipindi hiyo hata simjui kwa sura nikasema atakayekuwa brazameni
tu humu ndani ndio yeye, huku basi linaenda niligonganishana naye macho
akasmile nami nikasmile, nikamfata nikamkabidhi cd ikiwa na nyimbo
zangu 2 nilizirekodi kwa marehemu Mr. Ebbo zamani sana Motika Record!!!
MUNGU AMREHEMU!!
"Braza ngoma zangu hizi samahani
naomba kanipigie zipo poa sana na Tanga zimekubalika mno samahani sana
kanipigie", akawa ananisisitiza poa zimefika kama kali zitapigwa, we
shuka uwahi shule maana basi linazidi kwenda, nikashukia majani mapana
kule kutokea standi!!!
Hazikupigwa zile ngoma na msoto ukaendelea kama kawa!! nadhani hazikuwa na kiwango bora au mimi sikuwa mkali!!!!
2. MWAKA 2007 nilirecord nyimbo yangu
ya kwanza SALUTE kwa producer Abbuy wa Tanga, Studio za GOMBA RECORD,
sasa wakati naipeleka Dar kwenye vituo vya redio nikakutana tena na B-12
akaniunganisha kwa Dj Nelly ambae alikuwa mjengoni kipindi hicho kama
mmoja wa watu waliokuwa wanafanya kitengo cha muziki pale Clouds Fm.
Basi nikafika mjengoni kitega uchumi
pale mchana mapema nimeambiwa nifike saa kumi mimi nimefika saa tisa,
adabu za kale mbele hapo, kufika nje nikamwambia mlinzi nataka kumuona
B-12 nina ahadi naye, daah nilipewa mkwara, nikaambiwa nikamngoje chini.
Sijakaa sawa mara bwana Matonya naona
anapita pale na anaingia ndani bila bugudha kwa mlinzi, kidogo tena
nikamuona A.Y naye akapita bila kuulizwa lolote, daaah moyoni nikawa
natukana kimoyomoyo.
Baadae B-12 akatoka akanipeleka hadi
kwa Dj Nelly, ilikuwa kama oyaa Dj Nelly msikilize huyo mdogo
wangu...dah jamaa akawa kama hasikii vile apo nimesimama na kacd kangu
pembeni nashangaa tu kumbe huyu ndiyo Gadner na huyu ndiyo P.J okey hapo
Jahazi ndiyo linataka kuanza.
Dj Nelly akaanza kusema 'oya sema
shida yako?' nikajibu aaah braza mimi naitwa Ro.... akanikatisha haraka
na kuniambia nina dakika 2 tu za kuongea naye, kisha akachukua CD
akaiweka kwenye machine vile inaanza tu akaisimamisha hakuicheza tena,
na hapo yani kaisikiliza nyimbo ndani ya sekunde 15 au 20 akaitoa CD na
kunijibu hamna kitu Production mbovu na huwezi kuchana!!! kisha
akamgeukia Gadna na kuendelea na hadithia zao, mimi nikamuuliza sasa
braza nishauri nifanyaje? Oyaa dogo tuna maongezi hapa huoni!!? hatuwezi
kupiga nyimbo kama hiyo akanijibu kwa ukali... dah nikakosa pozi
nikaanza kusepa, huku moyoni najisemea, aah wewe Gadna si ni Mtanga
mwenzangu wewe hata hutii neno kaka?.
Nikamfata B-12 wangu maana ndiyo
alikuwa kimbilio langu mjini hapa, naye hakuwa na jinsi wal anamna ya
kufanya maana hawezi kupiga nyimbo kama kitengo cha muziki hakujaruhusu,
akanishauri nikairudie nyimbo ile kwa Dunga... kipindi hiyo Dunga
alikuwa ndiyo gumzo.
Hivyo nikatoka pale nikaipeleka ngoma
ile ile East Africa Radio nikaiandikisha na nikasepa hapo nauli
inaelekea kuliwa, babaako nikalirudisha kunani Tanga moja.
Aaah! East Africa Radio bana
wakanipigia simu na kusema nyimbo yako tunaitambulisha leo na wana
segment inaitwa ipotezewe au iendelee kuwepo kitu kama hicho... basi
nikiwa Tanga nikatega sikio kwenye satelite kusikiza baadae wakaipiga na
ikapata kura 338 zikisema iendelee kuwepo na kura 34 zikisema ipotezewe
nakumbuka hadi leo hiyo!!! basi nyimbo yangu ikapita na ikawa inapigwa
pigwa east East Africa Radio.
Wakati huo huo samahani kabla
sijaenda Tanga, nikiwa Dar nilikutana na Jaffarai alikuwa ni rafiki wa
karibu wa braza yangu, braza akanitambulisha "Huyu mdogo wangu anaitwa
Ebra au ROMA anarap na kaleta nyimbo yake"... hapo natamani jamaa aseme
tuisikize... (si unajua zile ukiwa unajiamini na nyimbo ni nzuri) basi
tukamshawishi aisikize, basi tukaenda kwenye gari na akaiweka.
Uwiiiiiiii! Jafarai akaanza "Aaah
mbona anachana kama mwana FA? aaah! hana style yake huyu babu, tafuta
style yako mzee, game gumu mzee, njoo kivyako man", sasa nikawa
najiuliza nachana vipi kama Mwana FA? mh! nikaona ananikata tu
nikamchana braza tuondoke bwana naona navurugwa tu. Tukaaga tukaondoka
kinyonge!!
3. MWAKA 2008 nimeshajichanga nipo
safi ndiyo nakuja Dar rasmi sasa kurekodi TANZANIA hapo nimeshaongea na
Nahreal, na pia nakuja kuirudia ile ngoma iliyokataliwa radio nakuja
kuirudia kwa Dunga.
Ndipo hapo tukiwa na braza mitaa ya
mikocheni nadhani. Ndio tunakutana na Fid Q, Jafarrai na Mussa Hussein
wa uswazi yule, tukafika na kaka hadi pale tukasalimia pale ila si
unajua kisanii mara nyingi ukimsalimia mtu ni kama anakuwa anakukataa
hivi anaitikia short short ndivyo ilivyokuwa.
Sasa kaka akaanza kuongea na Jafarai
mambo yao tu aaah! katikati ndiyo wakachomekea kaka akamwambia Jaffarai
"Aah! tunaenda 41 Record kwa Dunga nampeleka mdogo wangu huyu si
unamkubuka"?? Jafarai akajibu aaah! huyu si yule wa kipindi kileee? hapo
ujue mwaka umeshapita hapo, kaka akamjibu ndiyo huyu sasa amekuja
kuirudia ile ngoma huku kwa Dunga!!
Jafarai akasema aaah amebadilika? au
bado anachana vile vile? dogo badilika aisee! game gumu sana dogo kwa
style ile unapoteza hela tu huwezi kutoka, sasa akaanza kunivuruga tena
ila moyoni nikawa nasema " Mbona Fid Q haununui huu ugomvi? yani kwanini
haulizi lolote daah! hapo Fid Q kajikausha hata hatusikilizi yani yeye
busy wanaongea na Mussa tu, mimi nikawa natamani kaka aseme kitu tu.
Hatimaye Fid Q akaingilia "Oya kwani
vipi babu? mbona kama unamnyea sana jamaa"? akamuuliza Jafarai? Jafarai
akajibu "Aah! huyu dogo alikuja huku kama mwaka umepita hivi, akaniletea
nyimbo yake, ila ni ya kiwaki!! sasa kaenda kujipanga na sasa karudi
rasmi...
Fid akasema niaje babu? unaimba au
unarap? nikamwambia narap!! akasema ok 1,2,3 twendee... mamamammama
ndiyo nilichokisubiri kwa muda mrefu hiki.
Nikaanza kuchana nyimbo ile
iliyokataliwa radioni na iliyopingwa na Jafarai... sasa kadri
ninavyozidi kuchana naona jinsi bwana Kubanda anavyozidi kunogewa,
namimi naongeza misifa hapo nachana tuu kwa hisia.
Ikawa poa sana kwake na akakubali
hadi kuamka kwenye kiti na kunipongeza kuwa am good, lakini moynoi
nikawa nataka nimchanie TANZANIA maana ndiyo nimekuja kuirekodi na ndiyo
nina mzuka nayo na ndiyo naiona ni nyimbo kali, yani zile za (kama
kadata nahii tu je Tanzania nikichana itakuwaje)? sasa nikamwambia ngoja
nikuchanie nyingine... akakataa akasema aaah! mimi sitaki nyingine,
nichanie hii hii iliyokataliwa.
Sasa nikapita nayo tena. Sasa ujuee
na nyimbo hiyo ninayochana hapa ndiyo baadhi ya mashairi yake yamepita
tena kwenye MATHEMATICS na MECHI ZA UGENINI... niliyarudia kwa vile
sikutaka yapotee bure vitu kama "Ndoto zangu kitambo zilikuwa nije kuwa
padre, zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa weed etc.
Basi Fid Q alikubali sana na hapo
ndipo akasema una IQ sana bab...ndio chanzo cha ule mstari wa kusema
"Nawazidi kwa IQ shahidi Fareed Kubanda"! ambapo tazama sasa nimeuimba
kwenye ngoma ya 4 toka niambiwe hivyo na yeye.
Basi alikubali sana na akasema ni
bora nikarudie kwa Macko Chali na akawa anampigia simu sema Marco
hakupatikana akaniachia namba yake, sasa Jafarai na yeye alipoona Fid Q
anakubali akawa na yeye anasema aah! dogo sasa amebadilika sasa hahaha!
moyoni nikawa na furaha sana unajua inavyokuwa unakubaliwa na watu kama
hawa kwa kipindi hicho u konw it!! nikaondoka na kaka tukawaacha
majamaa, nikaendelea na hasso za kurekodi kwa Dunga na Nahreal!!!
HIZO NI BAADHI ZA MICHONGO ILIYOHAPPEN KABLA HAIJATOKA WALA KUREKODIWA NGOMA YA KWANZA YANGU ILIYONITAMBULISHA "tanzania"
4. BASI YAPO MENGI SANA YANAJAA KITABU NADHANI NA MENGI NI YA KUSISIMUA.
NATAMANI NIPATE INTERVIEW TENA YA TV HARAFU NIHADITHIE KWA SAA MOJA NA ZAIDI YOTE HAYA.
SEMA YOTE HAYA UTAYAPATA KWENYE
"DOCUMENTARY YA ROMA 2030" KUANZIA NAZALIWA HADI HAPA NILIPO SASA.
(UZURI NI KUWA KUNA BAADHI YALIREKODIWA SO ITAKUWA IPO REAL SANA).
TUENDELEE KUNGOJA!!! NAJUA MNAENJOY NIKIFUNGUKA HIVI YAPO MENGI KAMA;
1. Mimi kukutana na kala na kugonganisha mawazo ya wimbo wa Tanzania na wa kwake wa wimbo wa Taifa.
2. Nakaaya kunizingua kwenye
kumshirikisha katika ngoma yangu ya Tanzania, ila badae alinitafuta na
kuniomba kolabo baada ya kutoka Mathematics.
3. Wasanii wakubwa kunikatalia kwenye
kolabo zangu kama Mr. President na Tanzania, ndiyo maana nasimama bila
kumshirikisha mtu kiivyo.
4. Nikki wa Pili alisababisha nikarekodi mechi za ugenini though yeye hajui hili.
5. Nilivyoingia kwa Duke M. LAB na
kurekodi Mr. President lakini haikutoka, na mimi nikahamia Tongwe na
kuanza kurekodi upya hadi leo nipo Tongwe.
6. Nilihit sana na Tanzania lakini
Jay MO aliwahi kuniambia hanifahamu... ila siku zikaenda akaja
akanifahamu na tukafanya naye MVUA NA JUA REMIX kwa majani.
7. Kwanini wadau wengi wakati natoka
na Tanzania hadi Mr. President walinambia THAT IS HIP HOP!!! safi kaza
mwana harafu leo inatoka hit kama Mathematics wanasema sifanyi hip hop!!
napayuka!! naropoka!! napiga makelele!! sina stye!! na mengi tu hadi
kusema tuzo sikustahili.... duuuh! HATARI AISEE!
8... NYIMBO YANGU YA TANZANIA
ILIVYOKATALIWA NA RADIO STATIONS NYINGI, ADAM MCHOMVU ALIKUWA MBISHI
SANA THANKS GOD AKAIPITISHA NA RADIO ZA MIKOANI ZIKASSUPORT MNO!!
..9.......10.....
Nawapenda sana watu wangu kuna vita
kubwa sana dhidi yetu basi katika sala zenu msinisahau kuniombea niwe na
afya njema na maisha yenye heri na baraka na marefu mimi na familia
yangu na Tongwe wote na ndugu jama na marafiki wote!!!
No comments:
Post a Comment